Hii ndoa inaanza kuwa ngumu kwangu, nawaza kufanya hivi

Haya bwana tumekusikia, lakini kumbuka hakuna mkamilifu chini ya jua, kila mmoja ana mapungufu yake la msingi ni kuvumiliana tu,

kwanza mmekutana ukubwani kila mmoja katoka kwao na malezi yake, hivyo hawezi kuwa kama unavyotaka wewe, labda umuumbe wako.

Ndoa zote ziko hivyo mkuu tunavumilia tu.
 
Nawaza kutafuta mchepuko mkuu
Je itanisaidia kupunguza stress? Maana mke wangu nimeshakaa nae nikamwambia lakini ataelewa leo kesho yaleyale mkuu
Mkuu kabla hujamuoa hukujua hizo tabia zake au ulijua ukimuoa utazivumilia na yeye atabadilika?

Mchepuko sio sululisho la tatizo la mkeo, tafuta njia nyingine tu
 
Hayo mapungufu hukuyaona kipindi cha urafiki wenu?,au mke umetafutiwa na wazazi?,
 
Mhhhh. Hii akiiona DIVA lazima aiibe,
Any way
Mkuu mimi kwa upande wangu naona hapo. Umelamba garasa,
Ngoja wajuzi wajeeee.
 
nikwambie tu!
KILA MTU ANA MAPUNGUFU YAKE!
KAA CHNI NA MKEO MUORODHOSHEE YOTE UNAYOONA YANAKUKERA!
AKIWA NA AKILI ATAJIONGEZA!
as for kuwa na mchepuko!
hakuna mtu atakwambia uwe nae au usiwe nae na we ukaamua kuwa nae au kutokuwa nae ukasema niliambiwa JF!
NI MAAMUZI YAKO!
Halaaaafu wakati anapanga bajeti mpk senti ya mwisho hizo hela anakuwa amezishika mkononi au?
na ye ana kipato?
kama anacho mwambie atumie chake kufanyia huo hayo maroroso yake!
zako fanyia mambo ya msingi!
kama ya msingi yanahusisha gharama za mchepuko ,GO AHEAD!
 
 
Mkuu usichepuke tafadhali kama dini yako inaruhusu kuwa na mke zaidi ya mmoja bora uhalalishe kwa kufuata taratibu za dini yako.

Maradhi mengi sana siku hizi usije ukawaacha watoto wako wakiwa yatima kwa ajili ya kukosa maarifa ya kufuata njia stahiki.

Ndoa zina mitihani mingi sana mkuu ila yakikufka shingoni hakuna jinsi kwa sababu hata uvumilivu unamipaka yake so usijetese sana kwenye ndo kwa kuhofia kelele za walimwengu. Hataki kujirudi wala kuenenda na tabia njema za wanawake wema piga chini songa mbele hiyo habari ya kutenganishwa na kifo itakutokea kwa sababu huyo mwanamke ndiye atakaye kusababishia kifo.
 
kwanza useme ukweli mkuu maana mtu aliye kwenye ndoa kuongea haya naona ugumu tena ndoa ya miaka mitatu kuwa mkweli ndugu yangu
imani inanituma hujaoa
 
Kila mtu ana mapungufu yake kikubwa ni kuvimiliana tu, kuchepuka sio kutoa tatizo ila ni kuongeza tatizo

Hata wewe una mapungufu yako ila anakuvumilia, usione wazee wamefika mpaka uzeen ukawatamani, wamevumilia mengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…