Hii ndoa inaanza kuwa ngumu kwangu, nawaza kufanya hivi

Haya bwana tumekusikia, lakini kumbuka hakuna mkamilifu chini ya jua, kila mmoja ana mapungufu yake la msingi ni kuvumiliana tu,

kwanza mmekutana ukubwani kila mmoja katoka kwao na malezi yake, hivyo hawezi kuwa kama unavyotaka wewe, labda umuumbe wako.

Ndoa zote ziko hivyo mkuu tunavumilia tu.
 
Nawaza kutafuta mchepuko mkuu
Je itanisaidia kupunguza stress? Maana mke wangu nimeshakaa nae nikamwambia lakini ataelewa leo kesho yaleyale mkuu
Mkuu kabla hujamuoa hukujua hizo tabia zake au ulijua ukimuoa utazivumilia na yeye atabadilika?

Mchepuko sio sululisho la tatizo la mkeo, tafuta njia nyingine tu
 
Mhhhh. Hii akiiona DIVA lazima aiibe,
Any way
Mkuu mimi kwa upande wangu naona hapo. Umelamba garasa,
Ngoja wajuzi wajeeee.
 
nikwambie tu!
KILA MTU ANA MAPUNGUFU YAKE!
KAA CHNI NA MKEO MUORODHOSHEE YOTE UNAYOONA YANAKUKERA!
AKIWA NA AKILI ATAJIONGEZA!
as for kuwa na mchepuko!
hakuna mtu atakwambia uwe nae au usiwe nae na we ukaamua kuwa nae au kutokuwa nae ukasema niliambiwa JF!
NI MAAMUZI YAKO!
Halaaaafu wakati anapanga bajeti mpk senti ya mwisho hizo hela anakuwa amezishika mkononi au?
na ye ana kipato?
kama anacho mwambie atumie chake kufanyia huo hayo maroroso yake!
zako fanyia mambo ya msingi!
kama ya msingi yanahusisha gharama za mchepuko ,GO AHEAD!
 
Habari zenu wana jamiiforums
Natumai mnaendelea na ujenzi wa taifa.

Najitokeza hapa kwa jambo moja ambalo linaniweka dilemma kwelikweli.
Iko hivi, Mimi ni kijana nimeoa Mke wang tumeishi takriban miaka mitatu katika ndoa ila kuna vitimbwi balaa, katika muda wote nimekua mvumilivu sana maana Mke wangu ana vimbwanga balaa, ana kero ndogo ndogo, ana maudhi mengi sana.
Simaanishi kua anachepuka hapana, ila huyu mwanamke ana mapuuza wawezi kupanga nae ratiba ya shughuli flani na baada ya muda anaibadilisha then ukimuuliza anasema ilitokea bahati mbaya , sasa hii hali imekua ikijirudia sana nishaichoka wakuu,
Mke wangu anapenda safari kama dereva aisee inaniboa sana hapendi kutulia kabisa kiguu na njia na huko kote ataleta hoja nyingi ili mradi apate ruhusa ila nishamjua ni mtembeaji.

Anapenda kuishi vizuri kuliko hali halisi ya kifedha iliyopo, hana plan ya kujibana ili tudundulize baadae tule bata kivulini, yeye Pesa iliyopo anaipangia bajeti mpaka ahakikishe inaisha yote hata kama vitu vingine havina umuhimu kununua, wote mnajua tunafanyaga mahitaji kwa kuangalia priorities sasa Mke wangu mimi majanga wakuu.
Mke wangu mgumu kuomba samahai hata akukosee ukimtuhumu utamsikia "aya" au yaishe baba flani wakati huo mi nishakua bored kweli kweli.

Sasa Mke wangu nimejitahidi kuishi nae kwa uvumilivu wa hali ya juu, sikuwahi kufikiria kumsaliti but kwa sasa naanza kuwaza kuchepuka ili akiwa ananikwaza naenda kwa mchepuko kutoa stress zangu maana hanaga kuomba samahani na akikuomba duh! Siku hiyo ujue ni siku ya kipekee sana.


Nimeanza kukubaliana na wazee na wanaume wenzangu wanaamua kuoa wake zaidi ya mmoja na wengine huamua kua walevi lengo hua ni kupunguza stress za kwenye ndoa.

Wakuu nawaza niwe na mchepuko ili nipate uwezo wa kumpuuza mke wangu anaponiharibia mood, maana nikiwa na kipoozeo mke wangu sitampa attention kubwa endapo atanikosea kama kawaida yake.

Ushauri nahitaji hapa:
Nawaza kutafuta mchepuko
Je njia hii itanisaidia kupunguza stress? Maana mke wangu nimeshakaa nae nikamwambia lakini ataelewa leo kesho yaleyale
 
Mkuu usichepuke tafadhali kama dini yako inaruhusu kuwa na mke zaidi ya mmoja bora uhalalishe kwa kufuata taratibu za dini yako.

Maradhi mengi sana siku hizi usije ukawaacha watoto wako wakiwa yatima kwa ajili ya kukosa maarifa ya kufuata njia stahiki.

Ndoa zina mitihani mingi sana mkuu ila yakikufka shingoni hakuna jinsi kwa sababu hata uvumilivu unamipaka yake so usijetese sana kwenye ndo kwa kuhofia kelele za walimwengu. Hataki kujirudi wala kuenenda na tabia njema za wanawake wema piga chini songa mbele hiyo habari ya kutenganishwa na kifo itakutokea kwa sababu huyo mwanamke ndiye atakaye kusababishia kifo.
 
kwanza useme ukweli mkuu maana mtu aliye kwenye ndoa kuongea haya naona ugumu tena ndoa ya miaka mitatu kuwa mkweli ndugu yangu
imani inanituma hujaoa
 
Kila mtu ana mapungufu yake kikubwa ni kuvimiliana tu, kuchepuka sio kutoa tatizo ila ni kuongeza tatizo

Hata wewe una mapungufu yako ila anakuvumilia, usione wazee wamefika mpaka uzeen ukawatamani, wamevumilia mengi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom