Hii ndiyo serikali ya Tanzania Bwana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ndiyo serikali ya Tanzania Bwana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by oba, Jan 31, 2012.

 1. oba

  oba JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwa uhakika, sakata la mgogoro kati ya madaktari na watumishi wa afya linaendelea kuchukua sura mpya baada ya bunge kujipitishia nyongeza ya posho zao hadi 200,000 huku serikali ikidai haina pesa ya kutekeleza matakwa ya madaktari katikati ya bajeti.
  Najaribu kufikiria kuwa hiyo nyongeza ya posho za wabunge kuwa imefanywa katikati ya bajeti au ilikuwa ni agenda ya siri ambayo haikuwekwa wazi wakati wa bajet.
  Nionalo mimi ni kuwa SERIKALI IKO TAYARI KUUA WANANCHI WAKE KULIKO KUSIKILIZA HOJA ZA MADOKTA na ktk hili sitawasamehe viongozi!
  Ningekuwa mimi ningefanya hivi kwa hoja za madokta;
  1. Ningeamuru ma intern doktaz wote waliohamishwa warejeshwe muh2 walipokuwa awali
  2. Ningewachukulia hatua viongozi wa wizara waliokuwa chanzo cha mgogoro na kuchangia mauaji haya ya wananchi na kwanza ningeanza na katibu mkuu kwa kumtimua kazi
  3. Ningemsimamisha kazi mkurugenzi wa Hosp ya muh2 kwa kushirikiana na katibu mkuu kuua watu
  4. Ningetangaza nyongeza ya poso za madokta hadi 40,000- half per diem
  5 Ningeamuru wafanyakazi wote wa afya wapewe green kadi za bima ya afya
  6 Ningeagiza mchakato wa mishahara na allowances za madokta na wana taaluma ya afya ziwe reviewed within a month na kurekabishwa
  7. Ningeagiza haraka kurekebishwa kwa huduma za afya na nyongeza za vitendea kazi kwa wagonjwa ikiwemo kuongeza vitanda vya wagonjwa na vifaa vingine
  8. Ningeagiza utaratibu uanze wa kununua mabasi ya wafanya kazi wa afya kwa kila hospitali ambayo yangewachukua na kuwarudisha makwao kila siku
  9. Ningeanza utaratibu wa kuwakopesha madokta magari ili kuwapunguzia adha ya kugombania na kubanana na wagonjwa wao kwenye daladala
  10. Ningewaomba madokta samahani kwa usumbufu niliofanya kama serikali na kisha ningewasihi warejee kazini huku mchakato wa kuyatimiza yote hayo ukiendelea
  Nawasilisha
   
 2. k

  kaudagaa Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  una mawazo mazuri, unaonekana huna njaa sana na siyo mbinafsi.hongera mkuu.
   
 3. w

  wamwala Senior Member

  #3
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Oba kiukweli hiyo ndo soln bt kwa nchi yetu hii ni ndoto za alinacha hilo kufanyika. Tatizo madaktari wakikubali kuingia kazini bila madai yao kutatuliwa wameshaula wa chuya. Ngoja tusubiri
   
 4. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hii ndo soln pekee, hata mkubwa ukikosea ukaomba msamaha busara huongezeka zaidi. But not our government
   
 5. Ngararimu

  Ngararimu Senior Member

  #5
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Hizo ni ndoto za alinacha ndugu yangu hao madactari hawana maana kabisa na laana ya mwenyezi mungu itakaa juu yao kwa roho za watu walizosababisha kupotea kwa kuingia katika mgomo. kwangu mimi huu ni uonevu kwa wananchi wanyonge ambao kodi yao ndiyo iliyowasdomesha madactari . wao wangeweza kutumia maarifa na nafasi walizo nazo katika fani ya utabibu kumtia adabu mtu yoyote yule anayehusika katika sakata la kuwabania maslahi yao akiwepo mkuu wa kaya mwenyewe kwa sababu hakuna binadamu yoyote aliye hai anayeweza kutamba kwamba anaweza kumkwepa dactari bana. hawa mimi kwangu ni makunguru tuu WANAOGOPA GOMBE(mafisadi) WANAONEA BUZI (walala hoi ) BANA
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nadhani Madaktari wana makosa zaidi kuliko Serikali na kama ni dhambi ya kuua, Madaktari watakuwa wa kwanza kuibeba maana wao niyo wataalamu na ni uhakika walifanya kiburi na makusudi kwa vile walijua serikali itawagwaya kuhofia vifo vya wagonjwa, Jambo ambalo kwa kweli ni kinyume cha maadili ya utabibu. Fedha za serikali siyo kwa ajili ya Maslahi ya Madaktari tu achilia mbali kuwa kuna watumishi wengi wa umma siyo madaktari tu. Kuna huduma nyingi za kijamii zinategemea pesa za serikali. Madaktari wetu watakuwa wapeponzwa na wanasiasa na wasitegemee kuwa kuna serikali yoyote duniani inapapatikia Madaktari pekee kisa eti wanashikilia uhai wa watu. Ni dhana potovu na hata wakishika madaraka hao wanasiasa wanaowaponza. Zaidi ni kushusha hadi ya taaluma yao
   
Loading...