Hii ndiyo sababu ya wanawake wengi kuibua mabomu…!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Black+couple+arguing-378x300.jpg


Mnamo mwaka 1973 Dk. Paul MacLean, mtafiti toka taasisi ijulikanayo kama National Instute of Mental Health, alibaini kwamba, ubongo una sehemu tatu zinazoendana na nyakati tatu za mabadiliko ya kimaumbile.

Sehemu ya kwanza inaitwa reptilian. Hii inahusiana na kukutana kimwili kati mwanamke na mwanaume na tabia ya ukatili, hisia za hasira na hofu. Sehemu ya pili ni limbic brain. Hii inahusika na mapenzi, huzuni na wivu.

Hata matumaini asili yake ni katika sehemu hii. Sehemu hii ndiyo inayodhibiti mapigo ya moyo na joto. Yote haya huathiriwa na kuwepo mahali hapo na mtu tunayempenda. Hamu ya mapenzi huenda moja kwa moja katika sehemu hii. Ni sehemu ambayo ina pupa na inaenda kasi kama umeme.

Ni enao ambalo halitaki kabisa kujishughulisha na mambo ya kutumia akili au tathmini. Sehemu ya tatu ya ubongo inaitwa neo-cortex, ambayo huruhusu matumizi ya mantiki, kutafakari kwa kina, lugha, kufanya mipango, kufikiri na maamuzi ya kina baada ya kufikiri kwa kina.

Katika kitabu chake cha The Emotional Brain, Joseph LeDoux anasema kwamba, sehemu zile mbili za kwanza za ubongo zinathibiti sana ile sehemu ya tatu. Na wala hii sehemu ya tatu haina udhibiti kwa zile sehemu mbili. Na ndiyo maana katika maisha ya kawaida, ‘hisia hudhibiti fikra.'

Ingawa fikra zinaweza kuamsha hisia kirahisi, lakini fikra zinapata tabu sana kuziondoa hisia zikishaingia. Hii ina maana sehemu ya pili ambayo ndiyo inayoziamrisha hisia, inaweza kuiburuza sehemu ya tatu kila inapotaka. Limbic ya mwanamke itamwambia, "umempata mwanaume barabara." Sawa, lakini mwanaume mwenyewe ni mlevi..!
Limbic itasema, "Nitaishi naye hivyohivyo. Ana sura nzuri mno, ninajisikia vizuri sana ninapokuwa naye…."

Sasa nafikiri unaweza kuona kwamba, hata kama mwanamke anaweza kusema kwamba anamtaka mwanaume mwenye haiba nzuri na mtu mwema si lazima kwamba, ndiye atakayevutiwa naye. Mfano mzuri wa jambo hili ni chakula.

Je huwa tunakula chakula kufuatana na ubora wake kiafya? Hapana…! Wengi wetu tunakula kutokana na utamu na ladha ya chakula! Dona ni bora kuliko ugali wa mahindi yaliyokobolewa kiafya. Lakini asilimia 90 ya Watanzania wanapenda ugali wa mahindi yaliyokobolewa maarufu kama Sembe.

Hali hii ndiyo inayompata mwanamke anapofanya uchaguzi na kujikuta akimchagua mwanaume anayemfanya kujisikia raha, lakini ambaye si mtu mzuri kwake.

Suluhisho la jambo hili ni nini….?

Wanawake wanaweza kufanya urafiki na wanaume hao wazuri wa sura na wenye sifa ya uburuzaji na valuvalu kwa idadi wanayotaka kama kwa kufanya hivyo watajisikia raha maishani mwao; ili mradi tu urafiki huo usilete maumivu na huzuni ambayo yako juu kuliko furaha yenyewe.

Kama huzuni ni kubwa kuliko furaha katika mapenzi na mwanaume aliye naye, basi mwanamke hana budi kuachana na limbic brain na kuchagua mwanaume anayemfaa kwa kutumia mantiki.
 
aahh hunishindi mimi mi mpaka nakaribia kukusahau ila kitu kimoja siwezi sahau...

tukikutana itabidi tanesco wazime umeme ili isitokee shoti kwa jinsi tulivyomisiana

hahahahaaaaaaa...........kitu gani bana we acha uzushi!!! usijepigwa plasta kwa kunirandia! si unajua siku hizi kuna mabazazi yahooonga wake za watu!!! Careful ooh!!!
 
aahh hunishindi mimi mi mpaka nakaribia kukusahau ila kitu kimoja siwezi sahau...

tukikutana itabidi tanesco wazime umeme ili isitokee shoti kwa jinsi tulivyomisiana
......................................mh????????
 
hahahahaaaaaaa...........kitu gani bana we acha uzushi!!! usijepigwa plasta kwa kunirandia! si unajua siku hizi kuna mabazazi yahooonga wake za watu!!! Careful ooh!!!

ntakuambia tukionana uso kwa uso mwili kwa mwili.......

msafara wa mamba kenge hakosi hao bazazi wanaibiwa buree siku hizi kila mwanamke anasema kaolewa hata kama hana mchumba pete si zinauzwa tu kwahiyo aliyetoa cheni bandia nae kapewa pesa bandia
 
hiyo ya kuzima umeme hiyo ndio imenipa ulizo

aahh unajua msipoonana kwa muda mrefu miili inakuwa kama inapata shoti siku mkikutana soo inabidi tanesco wazime umeme wao usijezidisha mlipuko..

jina lako linanifurahisha
 
Mh! kaka Mtambuzi naona umeamua kutusuta leo, Loh! Haya bwana tunashukuru, maana huwa tunaambizana kuwa tafuta mwenye sura ya kutazamika ili ukikutana na mashosti zako ukiwatambulisha wakubali kuwa umepata mwanaume kifaa, kuliko unapata mwanaume ana sura nzitoooooooooooo! kama...PM wetu...! Naogopa kumtaja nitafungwa bureeee!
 
Napata shida, U handsome kwangu umekuwa kero, nitaanza kuvaa masks kama late Michael Jackson.
 
Back
Top Bottom