GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,044
- 119,617
- Ikitokea ajali mbaya na ya kizembe halafu DEREVA akawa bado yupo hai huyo dereva anyongwe hapo hapo ndani ya saa 24.
- Ikitokea ajali mbaya na ya kizembe ambayo kuna ABIRIA wengine wamepona na wakitoa ushuhuda wao wanasema dereva alikuwa mwendokasi basi hao abiria wote waliobaki wapigwe viboko vikali sana sita ( 6 ) au watembee kwa miguu kutoka hapo eneo la ajali hadi huko waendako. Kwani nilichokigundua katika moja ya watu muhimu wanaosababisha hizi ajali ni sisi abiria yaani mimi na wewe na wengi wetu hufurahia mno spidi zile huko njiani kiasi kwamba tukiona gari halikimbii " tunamnunia " na kuanza " kumdharau " dereva.
- Kama ajali ikitokea kutokana na ubovu wa barabara husika ambayo pengine imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kwa muda mrefu basi wahusika kuanzia WAZIRI wa WIZARA husika, SUMATRA na TANROADS Mkoa wote wahukumiwe kifungo cha maisha jela.
- Kama ajali ikitokea eneo ambalo kuna Matrafiki au Matrafiki muda mfupi tu uliopita walilikagua hilo basi ambalo pengine lilikuwa na matatizo ya kiufundi lakini kwa tabia yao ya kupenda rushwa wakaliruhusu basi kuanzia Kiongozi wa Trafiki wa Mkoa husika na wale Matrafiki wote wa zamu wanyongwe ndani ya saa 24.
- Kama ajali ya kizembe ikitokea na ikajulikana kuwa lile basi lilikuwa na matatizo ya kiufundi ya muda mrefu na Mmiliki wake anafahamu ila kwa kudharau tu na kutudharau sisi abiria akatupuuza basi Mmiliki wake apelekwe kati ya Mto Ruaha au Kagera au Mara ambapo kuna Mamba wengi na wenye hasira kisha " arushwe " tu hapo awe kitoweo chao " murua " cha siku.
Mamlaka husika ichukueni hii na ipo siku mtakuja kunikumbuka kwa wazo langu hili kwani tumechoka na Ndugu, Marafiki na Watanzania wenzetu kupoteza maisha kwa uzembe tu wa Watu wachache wasiojitambua na kujali maisha ya Watu.
Ajali ya Singida imenipandisha sana na mno hasira!