mmh....wanabariki ndoa? Sasa hapo wanakuwa wanabariki ndoa ipi wakati ndo wanaapa na kuvaa pete kwa mara ya kwanza?Nimeongelea mambo ya mimba wakati wa kufunga ndoa, kuwa na mtoto nje mmmhh, hilo ni suala lingine mkuu.. kwa mimi mkristo najua hufungi ndoa bali unabariki ndoa
Sidhani kama hiyo ni sababu. Mnaweza mkatest na bado tatizo likatokea mkiwa ndani ya ndoa, je hapo inakuwaje? Hiyo test yenu inakuwa na maana gani? Btw, mbona hiyo test ya kuonyesha uwezo wa kuzaa hata hospitalini inafanyika?Pamoja na kuhakikisha kuwa wote mnaweza kuzaa hii pia husaidia kujua kama mnaendana kimaumbile,sio ile baada ya ndoa mwanamke anadai huyu mwanamme simuwezi au mwanamme anadai kwa huyu dada naelea tu.
Jamani jaman, nimekuwa nikishuhudia wanandoa wengi wanafunga ndoa huku tayari mwanamke akiwa na mimba. Unakuta harusi fasta fasta inatangazwa na watu wanafunga ndoa, miezi mitano au sita unaambiwa fulani tayari ana mtoto, sasa wanapowahi kufunga ndoa lengo eti ni kwamba mtoto asizaliwe nje ya ndoa? jamani maana ya ndoa ni nini?
Imebidi nifanye utafiti mdogo na haya yamekuwa ni majibu ya baadhi ya watu:
1. Eti wanaume huwa wanataka kutest kwanza kama mke mtarajiwa anaweza kuzaa, na pia hata yeye kama anaweza kumzalisha mwanamke(a.k.a test before use) kwa hiyo asipopata mimba??..................................
2.Eti wanawake sio waaminifu, kwa hiyo ni kheri umpe mimba ili ujihakikishie kuwa sasa yeye ndo mke wako.
Sasa jamani tusaidiane ni kweli kuna maantiki ya kufanya majaribio? na je hiyo ndio dawa? NAWASILISHA
Mkuu nimesisitiza sababu yangu ya pili yaani siku ya ndoa mke kudai mchi hauwezi au mume kudai kinu kikubwa.Sidhani kama hiyo ni sababu. Mnaweza mkatest na bado tatizo likatokea mkiwa ndani ya ndoa, je hapo inakuwaje? Hiyo test yenu inakuwa na maana gani? Btw, mbona hiyo test ya kuonyesha uwezo wa kuzaa hata hospitalini inafanyika?