Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,198
- 7,536
Kimsingi mshikamano na ushirikiano wa hali ya juu "Team work" ndio nguzo muhimu zaidi ya zote kwa taasisi yeyote ile au watu wenye lengo moja na wanao pambana kuliendea lengo hilo.Ni kwa mshikamano na ushirikiano tu, watu wanaweza kulinyanyua jiwe kubwa ambalo kimsingi kama akijaribu kunyanyua mtu mmoja mmoja (mmoja baaada ya mwengine), wote wataishia kutenguka migongo na jiwe li pale pale.Ni kwa ushirikiano na mshikamano tu; Nyuki wanaweza kutengeneza asali ya kuwatosha kwa matumizi yao na nyingine nyingi ya ziada kwa matumizi ya viumbe wengine.
Hata hivyo ni lazima umoja na mshikamano huo utawaliwe na dhamira njema, upendo , njia na maono sahihi juu ya kule wanakotaka kwenda, kinyume chake itakuwa ngumu kufanikiwa.
Hata hivyo ni lazima umoja na mshikamano huo utawaliwe na dhamira njema, upendo , njia na maono sahihi juu ya kule wanakotaka kwenda, kinyume chake itakuwa ngumu kufanikiwa.