Hii ndio serikali ya ubungo mataa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ndio serikali ya ubungo mataa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Sep 20, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Sep 20, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  SERIKALI YA UBUNGO MATAA
  Nilikuwa kwenye kituo cha basi ( standi ya mkoa ) asubuhi nikasimamisha taxi ambayo ilikuwa inatokea ubungo kwenda shekilango , nilipoingia ndani ya gari mara vijana 2 wakaja , mmoja akaaa nyuma ya gari yule wa mbele akamfuata dereva akamlazimisha ampe shilingi 500 za kupakia , dereva akabishana nae lakini mwisho akampa , tulienda na gari mpaka magomeni ndio dereva akashituka tairi la nyuma moja halina upepo .

  Wakati anabishana na wale vijana mmoja alaingiza spoku kwenye tairi moja ya gari kama adhabu yake ya kubishana wakati wa kutoa pesa , kama wasipofanikiwa kutoa upepo basi kiongozi wao mmoja anaweza kuja kumchapa makofi dereva , pamoja na unyanyasaji mwingine .

  Hapo hapo wale wanaopanda dala dala wanajua vituko wanavyokutana navyo kama vijana wengine wanaokaa kituoni hapo zaidi ya masaa 2 kusubiri gari wanapopata hilo gari anaweza kwenda kushuka kituo kinachofuatia zaidi wanapenda kushuka mahakama ya ndizi au manzese tiptop , wakishafanya hivyo ujue ndani ya ya gari lazima kuna mtu atakuwa kaibiwa mali yake .

  Kuanzia Asubuhi na mapema kuna kuwa na wafanyabiashara mbali mbali eneo la ubungo mataa , muda wa asubuhi wengi wa wafanya biashara ni wale wa magazeti na vifaa vidogo vya magari ambavyo ni rahisi kubebeka pindi askari wa jiji wanapovamia eneo hilo , kuna wengine wanaouza vocha za simu , kuna matapeli na kila aina ya wafanyakazi .

  Wale wote wanaofanya kazi za kuuza magazeti wenye vibanda vyao , wale wanaotembeza njiani , hutakiwa kulipa karo Fulani , sio kwa serikali bali ni kwa watu wengine ambao wachukua wajibu huo wa kukusanya hayo mapato bila ridhaa ya serikali , mfano mwenye kibanda cha magazeti huwa analipa kuanzia 500 mpaka 800 kwa siku .

  Madereva wa taxi ambao hupaki magari yao karibu na eneo hilo nao hutakiwa kulipa karo kwa siku , vile vile hao wanaochukuwa makato hao ni wababe wa maeneo hayo ambao wakishafanya uhalifu huo wanaenda kujificha katika mto ambao uko karibu na njia panda ya chuo au nyumba za karibu na mataa .
  Vijana pamoja na madereva wakikataa kutoa hizo pesa ni kupigwa , wanapopeleka malalamiko yao kituo cha karibu yaani ubungo standi , wahalifu hawa huwa wanakamatwa na kuachiwa baada ya dakika chake na tatizo huja kwa Yule ambaye alimpeleka mhalifu kutuo cha polisi atakuwa hana amani na eneo hilo tena ni kupigwa na kufanyiwa visa vingine .

  Kundi hili la vijana linaongozwa na watu 2 mmoja anaitwa Hemedi pamoja Tembo , hemedi ni mwenyeji wa maeneo hayo ya mataa inasemekana baba yake ana nyumba eneo hilo , na yeye ndio kiongozi wa kuendesha vipigo kwa wale ambao hawalipi hizi pesa .

  Kama nilivyosema huko juu hawa wanaopigwa na kulipishwa pesa hawadiriki kwenda tena kutuo cha polisi kwa sababu ya usalama wao , basi pale pale kituoni kuna maaskari ambao wanapokuwa na njaa huenda kwa vijana wengine ambao kazi yao ni kuuza vipande vya sabuni vilivyo mfano wa simu .
  Hawa askari kanzu wanajua kabisa sasa hivi Fulani ameshauza simu nae anaenda kupata mgao wake , na ndio hawa hawa unapouziwa simu bandia unapeleka kesi kwao .

  Biashara ya simu za sabuni mara nyingi zinakuwa na watu zaidi ya 3 , kuna mmoja ndio mwenye simu halali na ndio mmiliki wa simu , huyo ukimwona ni mtanashati amependeza anaishi mjini kwa shuguli hizo kukodisha simu yake kwa hawa vijana , halafu kuna wengine kazi yao kuangalia kama kuna yeyote anayewaona wanaitwa site mirror , halafu kuna Yule ambaye ndio ameshika simu bandia ni watu wenye uelewano mkubwa sana .

  Kama wamekuuzia ukafanikiwa kuondoka ukashituka mbeleni bahati yako mbaya au nzuri ila kama wamekuuzia ukawapa hela ukashituka pale pale manaa yake unaweza kugeuziwa kibao wewe , ukapigwa na kuitwa mwizi , unaweza hata kuchomwa moto .

  Hii ndio serikali mpya ya ubungo mataa – wahusika wachukue hatua dhidi ya makundi haya yanayozidi kuchipuka kila mara
   
 2. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Hii imekaaa ki Mafia Mafia hivi!
   
 3. M

  Magezi JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  kuna ukweli ndani yake lakini nadhani kuna exageration zaidi. Hata hivyo nashukuru kwa taarifa hii imefika.
   
 4. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hakuna cha umafia wala nini. Hao watoto wa hapa ubungo wanalindwa na watu tu. Dawa ni kuleta kikosi cha askari kanzu toka mkoa jirani na kusafisha wote hao. Cha msingi ni serikali ya hapo Mataa iwajibike tu kuhakikisha mambo yao hapo yanaenda vizuri. Wengi ni vijana wao kwa hiyo wanawajua fika wahusika wa mambo haya!
   
 5. M

  MC JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Hii habari ina ukweli

  Jumatatu nilipeleka gari kuosha pale kituo cha mafuta Ubungo mataa, wale vijana wa gereji wakati nawaachia gari wakaniambia Mtu yeyote akijitokeza anasema anauza Simu Usikubali hata kumsikiliza.
  Mimi nikamwambia mimi mwenyewe wa town siwezi kuibiwa hapa Ubungo, yule kijana akasisitiza niwe makini kwa kuwa watu hao wanambinu za ajabu.

  Ninapoona habari hii, naamini kumbe kijana yule alikuwa anaeleza kitu cha kweli, na kwamba kutakuwa kuna mbinu ya tofauti inafanyika pale ubungo kuwaibia watu na hata kuwasababishia matatizo wale walioshtuka.

  Shame on Jeshi letu la polisi na UWT
   
 6. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  mkuu unanikumbusha machungu natamani nilie, nakumbuka mwaka 2008 kama mwezi 11 isingekuwa busara za kondakta ningeumbuka, nilikuwa nimetoka ubungo NBC kuchukua pesa kama 210,000/= kwa ajili ya ada ya kijana, basi nikatoka pale nikachukua daladala, ila gari ilikuwa imejaa nikaona ngoja tu nipande bazi mkuu mle ndani nilibanwa hadi nikawa kupumua siwezi, kufika big-brother jamaa wakashuka, sikuwa na wazo kuwa kuna wizi umetokea, sasa wakati tunafika usalama konda akawa amefika anadai chake, du mzee kujisachi sina hata shilingi, kichwa chote kikaanza kuniuma, ikabidi nimwambie konda kuwa nimeibiwa bahati nzuri konda hata hakuleta utata akanielewa ila nilifadhaika sana siku ile
   
 7. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  kuna jamaa walemavu wapo pale stendi ni hatari sana, kama unapanda nao gari then ukabahatika kukaa nao siti moja hesabu umeumia, jamaa wezi hatari sana, iliwahi kumtokea jamaa alimpisha yule mlemavu akae kilichomtokea mwenyewe akakoma, ubungo noma sana
   
 8. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  kule ndani napo hapafai kabisa kuna wizi sana, kuna watu wanaofisi palepale utawala lakini wana dili za wizi, hii nimeiona jamaa alikuwa anauza simu kwenye gari ambayo ilikuwa inataka kutoka, yule mteja aliiona ile simu kabla hajapanda kwenye gari ila walikuwa wanashindana kwenye bei caha ajabu baada ya mteja kupanda kwenye gari jamaa akakubali kuuza ile simu, gari ilipoondoka jamaa akaona aiangalie simu yake mpya aliyonunua, kuiangalia kumbe sio simu ikabidi jamaa aombe dereva amshushe, dereva akamshusha pale makao makuu ya tanesco jamaa akarudi hadi kule ndani kwa bahati nzuri yule jamaa aliyeuza simu akamkuta, kwa kuwa yule jamaa alishakuwa na hasira za kuuziwa kanyaboya alipomkuta akaanza kumpandishia, ila kilichitokea watu wote tulishangaa pale ndani, yule mwizi akajifanya polisi mwenye cheo akapiga simu polisi wakaja akaanza kusema yule kijana amemzalilisha kwa kumuita mwizi, polisi wakampigia saluti yule mwizi wakamchukua yule jamaa hadi kituoni pale stendi hata hatujui iliendeleaje ila inasikitisha sana, tukashindwa kuelewa yule ni polisi kweli au ndio wale askali wanashirikiana na wezi
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  mhhhhhhhh.
   
 10. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hawa vijana ni hatari sana, hata polisi wanawaogopa japo wao polisi wana silaha. Silaha yao kubwa hawa ni kukuvizia sehemu unazopenda kupita, wanatembea na spoku za kuchomea nyama, wakikubabatiza wanaizaimisha kifuani upande wako wa kushoto.

  Kuna mmoja pale Kituo cha mwenge yeye alikuwa akiitwa "MLANDIMU", aliishawahi ua Konda kwa spoku kisa kanyimwa shs 50.

  Ukweli serikali inatakiwa iwashughulikia na njia pekee ni kuwajengea askari polisi kambi na kuwataka wote wakae kambini, haya mambo ya polisi kupanga manzese ndiyo yanawaogopesha kufanya kazi zao, kwani ukiisha onekana wewe ni mnoko basi ni target ya hawa vijana ukiwa katiaka mood ya kiraia.
   
 11. K

  Kibongoto JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2009
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Inamaana serikali inawaogopa vibaka? PM alipokwenda pale Ubungo stand mambo hayo hawakumwambia? Na hawa wenye biashara zao (mabasi,maduka,hoteli etc) pale ubungo kwanini hawashirikiani wakaondoa uozo kama huu? Hapa Bongo kuna mambo mengine tunaendekeza wakati yapo mikononi mwetu kabisa.
   
 12. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 6,997
  Trophy Points: 280
  nchi hii imeoza kabisa
   
 13. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  ni vema kama kuna mwandishi wa habari humo jamvini aka-print hii akameplekea kova, kama ufisadi umetushinda bna hili nalo lisitushinde
   
Loading...