Hii ndio misemo mikali kwa Kiswahili

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,664
Kuna baadhi ya misemo ni mikali sana na ni migumuu kuielewa japo mingine ni rahisi sana kuielewa lakini unajikuta tuu automatically umeipenda! Mrisho mpoto,zembwela na baadhi ya wana hiphop hupenda sana kuitumia na humfanya mtu afikirie! Wale madereva wa Magari makubwa ya mizigo na dalala huwa na Hii misemo nafikiri wao ndio wanao ongoza

Leo naomba kushare nanyi baadhi ya misemo ...sema na ww kwako upi ni msemo mkali kwako

1.Hata Bibi naye alikuwa Binti

2.Ukimuona kuku kwa mganga ujue Rangi yake ndio imemponza

3.Hata Ukiogelea Binadamu watasema unawatimlia vumbi

4.Ukiona Manyoya Basi kaliwa

5.Mlango mkubwa lakini unalindwa kwa kufuli dogo

6.Kitendawili si Deni ukishindwa nipe mji

Endelea na wewe
 
"Hivi unaishi ili ule au unakula ili uishi "

"Hawara hana talaka ukitaka unamupata"

"Heri kuwa Mbwa Ulaya kuliko kuwa mwana wa Nchi"

"Usingizi ndugu yake kifo,hivyo usipende kulala"

"Ukitaka inzi wasikufaate basi acha kula vilivyo oza"

"Baya lisilo ni dhuru ni jema lisilo na faida".
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom