Hii ndio Miji 10 ya hatari zaidi ya kuishi duniani, Afrika ipo miji 4

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,446
dunia2-660x400.jpg

Vitendo vya Ugaidi ni miongoni mwa stori zinazoshika na kuweka headlines kubwa sana duniani, na kwa sehemu nyingi za dunia vitendo hivi sio vya mchezo kabisa.
Kutokana na ukuaji mkubwa wa vitendo ya Ugaidi duniani, makosa kama wizi kwa kutumia mitandao, uhalifu wa IT na migogoro baina ya mipaka ya nchi ni vitu vikubwa sana, unaweza kusema hakuna nchi iliyo salama kabisa.

Nimekutana na orodha moja iliyo orodhesha Miji 10 ya hatari duniani, Miji 4 ya Afrika imetajwa, ungependa kuijuwa? Nimekusogezea picha zake hapa chini.

1. Afghanistan, Kabul

Hakuna idadi ya wanajeshi wa Kimarekani wanaoweza kuusaidia mji mkuu wa Afghanistan, Kabul dhidi ya matukio ya Kiagaidi nchini humo. Na huu ndio mji wa hatari zaidi duniani. Matukio ya mabomu, kulipuliwa kwenye mahoteli na Ubalozini ni kitu cha kawaida.

2. Somalia, Mogadishu

Mpaka hivi karibuni, Mji mkuu wa Somalia, Mogadishu ulikuwa moja kati ya miji hatari zaidi duniani. Umoja wa Mataifa walijiondoa kwenye ulinzi na usalama wa nchi hiyo baada ya Serikali tawala kuanguka mwaka 1991. Matukio ya Al Qaeda yalivuma mpaka mwaka jana ambapo wapiganaji wa Umoja wa Afrika waliingilia kati.

3. Iraq Baghdad

Iraq, Baghdad ni miongoni mwa miji ambayo sio salama pia na kwenye matukio mbalimbali ya Kigaidi hutokosa kulisikia jina lake. Lakini baada ya Marekani kuingilia kati matukio mengi yanayotokea mjini Baghdad hali kidogo imetulia. Miaka mingi ya matukio mbalimbali imeharibu miundo mbinu ya mji huo.

4. Ciudad Juarez,Mexico.

Mexico ni nchi inayofahamika kama bandari ya madawa ya kulevya duniani kupitia mji wa Ciudad Juarez. Wafanyabiashara wa madawa ya kulevya Mexico wanaogopwa na mapolisi wengi ni vijakazi wao wakubwa. Ciudad Juarez ni moja kati ya miji hatari zaidi duniani ukitoa maeneo yake ya vita.

5. Abidjan, Ivory Coast.

Abidjan ni mji uliopo Ivory Coast ambao kwa muda mrefu kulikuwa na matukio ya kialifu mengi sana yaliyoteka headlines mbalimbali duniani lakini baada ya kukamatwa kwa aliyekuwa Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo alievua majukumu yake kumpatia Rais aliyechaguliwa Alassane Outtara, Abidjan kidogo imetulia lakini bado unahesabika kama mji hatari.

6. Caracas, Venezuela.

Caracas mji mkuu wa Venezuela nao pia upo kwenye list ya miji hatari zaidi duniani na unahesabika pia kama bandari ya madawa ya kulevya. Makosa kama uwizi, kuporwa na makosa mengine madogo ni vitu vya kawaida sana kwao mapolisi hawana sauti wala nguvu ya kudhibiti vitendo hivi.

7. Sana’a, Yemen.

Mji mkuu wa Yemen, Sana’a umekuwa ukiingia kwenye headlines mbalimbali duniani kufuatia vita dhidi ya aliyekuwa Rais wa nchi Ali Abdullah Saleh. Mgogoro huo umefuatia na matukio kadhaa ya Kigaidi nchini humo na kuwekwa kwenye orodha ya miji hatari zaidi duniani.

8. Peshawar, Pakistan.

Pehsawar mji uliopo Pakistan ni miongoni mwa miji hatari duniani, mji huu sio salama kabisa kwa wageni matukio ya kutekwa na kulipuliwa na mabomu ni matukio ya kawaida sana kwao.

9. Nairobi, Kenya.

Matukio ya Al Shabaab nchini Kenya pamoja na matukio mengine ya kiualifu iliiweka Kenya kwenye headlines mbalimbali. Kutembea au kusafiri usiku nchini Kenya sio salama kabisa kwani kuibiwa na kuporwa ni matukio ya kawaida.

10. Cape Town, South Africa.

Cape Town mji uliopo South Africa ni maarufu sana kwa maeneo ya kitalii duniani, lakini ikifika usiku mji huu sio salama kabisa kwa matembezi haswa kwa wanawake. Matukio mengi ya uhalifu ni kutokana na ubaguzi wa matabaka kati ya matajiri na maskini.
 
Toa Abidjan na Nairobi and replace it with Jo'burg and Buja
 
Johannesburg haipo mnaweka Cape Town kweli wakati Cape Town unaweza kutembea usiku Long street kwenye maeneo ya club na Water front hiyo Jobeq kuanzia saa kumi na mbili jioni ni hatari kutembea...
 
hata Mimi nashangaa aisee cape town long street na water front kuna wale security guards jina limenitoka wahalifu wanawaogopa kinyama hivi jobeq kweli unaweza ukapita kwa kurelax mitaa ya Nugget au Jozi kweli!! hapo Nugget kudadeki unakabwa saa 6 mchana na wengi wa wahalifu mitaa hiyo ni watanzania halafu Nairobi ameionea aisee bora hata list angeinclude Lagos ,Nigeria
 
Nimeshawahi kuishi Johannesburg kila nikiufikiria mji ule malaria kichaa inanipanda gafla!wazimbabwe ni watu hatari sana kwa mji ule!unakabwa mchana kweupe kabisa bila msaada wowote!hata wabongo na wamalawi sio chochote!na ukienda Durban ndio wabongo kibao wanakaba hadi kimvuli na cape town wakabaji wengi ni Half cast,utakuta jitu linaonekana ni mzungu flani kumbe likabaji tu
 
Kuna movie inaitwa (13 HOURS:SECRECT SOLDIER IN BENGHAZI).hii movie inaonyesha jinsi gani mji wa Benghazi ulivyokuwa mji hatari zaidi duniani maana magenge ya waasi kila sehemu,kila wilaya ina uwongozi wake.mauwaji kila siku ni kitu cha kawaida mpaka sokoni watu wanauza nyanya huku wameshika bunduki.uki search huu mji kwenye google basi lazima utakuletea ujumbe kuwa huu mji sio mji mzuri wa kwenda kutembea au kufanya biashara.

balozi wa mwisho wa marekani kufanyiwa assasination ilikuwa mwaka 1979 nchini Afghanistan,toka hapo ulinzi ulimalisha kwa mabalozi waliyoko kwenye nchi husika.lakini imekuja kuwa ngumu ndani ya mji huu baada ya balozi wao kufanyiwa assasination mwaka 2012 na kuamua kufunga ubalozi wenyewe kwa sababu za kiusalama.ni mji hatari sana
 
Last edited:
Kuna movie inaitwa (13 HOURS:SECRECT SOLDIER IN BENGHAZI).hii movie inaonyesha jinsi gani mji wa Benghazi ulivyokuwa mji hatari zaidi duniani maana magenge ya waasi kila sehemu,kila wilaya ina uwongozi wake.mauwaji kila siku ni kitu cha kawaida mpaka sokoni watu wanauza nyanya huku wameshika bunduki.uki search huu mji kwenye google basi lazima utakuletea ujumbe kuwa huu mji sio mji mzuri wa kwenda kutembea au kufanya biashara
watu wanauza nyanya na bunduki sokoni
 
Back
Top Bottom