Hii ndio maana halisi ya Rasta

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Maana halisi ya neno RASTAFARIAN: Ni imani ya mtu mweusi au mweupe inayotetea UTU wa MTU MWEUSI. MPIGANIA HAKI YA MTU MWEUSI huitwa RASTAMAN au RASTAWOMAN na kwa WATOTO wao huitwa RASTABABY.

Imani "kamili" ya Rasta ilianzishwa zaidi ya miaka 100 iliyopita huku kundi kubwa la waafrika waliokuwa mikononi mwa wakoloni walipoweza kuingia kwenye imani hiyo huku nchi ya JAMAICA ikiwa na wafuasi wengi.

Dredy locks ni moja kati ya kitambulisho kikubwa cha Rastafarian, lakini si kila mwenye dredy locks basi akawa Rastafarian kwani asilimia 25 ya Rastafarian hawana Dredy locks na ndipo tunapoona kwamba kufuga dredy si kuwa na imani ya Rasta bali matendo humpeleka mtu kwenye imani ya Rasta.

Rastaman hupenda kujiajiri na mara nyingi hufanya shughuli zake kwa kutumia mikono na si vifaa vya kazi na kati ya kazi za Rasta ni SANAA, wao hufanya aina zote za sanaa lakini kazi zote hizi Rasta hujiajiri na si kuajiriwa.
 
Ukikutana na wale asilia utawagundua kwa urahisi sana, wapole, wana huruma, wastaarabu, hawapendi shari ila wapo wa kibongo ambao rasta kwao ni fashion..................
 
Movement yao ilitwa jina la RAS TAFARI kwa heshima ya Ras Tafari Makonnen ambaye alimpa/mtawaza Mtawala Haile Selassie wa Ethiopia mwaka 1930.

hata neno Rasta limetokana na neno Ras Tafari (watu wengi wanajua/tamka rastafari
na ndio maana watu wengi wa aina hiyo huitwa RAS (MARASI)
 
Back
Top Bottom