Itoye
JF-Expert Member
- Sep 29, 2017
- 531
- 1,024
Kheri ya Pasaka.
Hili sakata la Boss wa TPDC limeacha maswali mengi sana ambayo binafsi natamani Mh. Rais alitolee ufafanuzi ili kujenga imani juu ya mfumo wa mipango na maamuzi unaomsaidia katika kutekeleza majukumu yake?
- Sababu zipi alipewa hadi akaridhia kumtengua Boss aliyekuwa akihudumu?
- Kama aliziona zina mashiko na ni nzito, Je! Alijipa muda kujiridhisha juu ya ukweli wake? Je sababu hizo zimepoteza mashiko ndani ya muda usiozidi masaa 24? Au kama bado alikuwa hajajiridhisha kulikua na uharaka gani wa kutoa tangazo lile?
- Jambo hili limewezekana ku - "Undo" lakini naamini kwa muhusika kuna namna limemuathiri, Je! Lingekua ni jambo ambalo madhara yake huwezi kuyabadili au kuyafuta kwa urahisi au ambalo madhara yake ni ya kudumu wangekua tayari kuwajibika? Kama ni ndio basi hata ktk hili natamani kuona watu wakiwajibishwa.
Au tukio hili ndio linadhihirisha ukubwa wa tatizo la kukosekana kwa "network and coordination of information" kama Katibu Mkuu kiongozi alivyosema na Mh. Rais akakazia? Kama hivyo ndivyo basi tuna tatizo kubwa mbele yetu.
RIP JPM.