Hii ndio Desemba bwana

ndusu

Member
Sep 7, 2014
26
8
1.Mwaka ndio unaishia, utakuwa unatathimini uliyoyafanya tangu mwaka uanze, pengine unafurahia au kujutia, Mshukuru Mungu kwa yote, jipange kwa mwaka ujao.

2.Umejipanga kwa ajili ya Krismas?, umejichanga pesa ya kuwanunulia wanao/familia nguo za krismas, chakula kizur, maua, Chrismas tree?


3.Vipi una mpango wa kutoka kwenda mahali na mpenzi wako ,familia au marafiki?, labda beach, hotel nzuri, Mbuga za wanyama, kubadilisha mazingira, kula, kunywa na kufurahi?


4. Umepewa bahasha ya mchango wa krismas kanisani? Jiandae kumpokea kristo.


5. Umeshachukua likizo yako ya mwisho wa mwaka? Au ndo uko bize ofisini kuandaa ripoti za mwaka?

6. Mvua za vuli zimeshaanza, vipi umeandaa mashamba? Mda wa kupanda hauko mbali/ndo huu.


7. Januari haiko mbali, unaesomesha umeandaa ada ya watoto, na vifaa vingine vya shule; sare, michango ya madawati, walinzi, taaluma n.k? Labda kama una Junior Jumbo.

8. Bidhaa za discount (punguzo) zinakuja, umejipanga kuzipata?

9. Vipi mkutano wenu wa VIKUNDI/VICOBA wa mwaka umeshafanyika? Unakwenda kupata taarifa ya mwaka? gawio lako? au ndo unarudisha deni la mkopo uliochukua.

10.Mwaka unaisha, labda hata mkataba wako wako wa pango la nyumba ndo unakwisha, jichange umpe chake mwenye nyumba.


11. Au wewe uko side B, huu ndo msimu wako wa kupiga pesa kutoka kwa wale wanaozitumia, una duka la nguo? Vinywaji? maua? bidhaa mbalimbali, umejiandaa kuvuna? Umejipanga na ushindani kutoka kwa wauzaji wenzako.
Kama hata moja ya haya hayakuhusu, sijui utakuwa unaishi maisha gani?

Ongeza mengine
.
 
Back
Top Bottom