Hii nchi itakuja kuendela kwa namna gani

The hammer

JF-Expert Member
May 17, 2011
2,396
1,784
Wadau, hii nchi itaendelea kweli? Mbona naona kuna maigizo mengi sana kuliko uhalisia wa kutafuta hayo maendeleo?

Ona, je kuna mipango madhubuti yenye kuzingatia uchumi unaokuwa kwa weledi huko mbeleni? mipango hiyo ni ipi?

Je, matatizo ya wananchi yanashughulikiwa kweli kwa moyo wa kuondoa umaskini au ni ku-ng'ong'ana kwa pembeni?

Mfano, padri, mchungaji au Shekhe anafikiria nini anapopoteza muumini mmoja? Serikali inafikiria nini kuhusu biashara za watu kufa, watu kufilisika na hali ya manunuzi kupungua sana.

Tanzania tuna tatizo la wivu sana kuhusu maendeleo ya watu. Kuna mifano mingi sana.Diamond anapigwa vita na watu kwa ajili ya maendeleo yake mwenyewe.Thabeet naye ku-fall kwake kama kuna watu wanafurahia hapa, kuna Notherner hater,Yanga au Simba zikianguka watu wanafurahia, Miss-Tz hakukosa, Mbowe anaombewa afilisike, wa magazeti ya Ijumaa wikienda (kama sijakosea) naye watu walitaka aisome namba.... Je Watanzania shida yetu nini? Kupata maendeleo au kushushana maendeleo? Ili kila mtu ajue ana maadui Mil. 45+

Je,serikali imeingia katika huu wivu wa watu wake ambapo ingewasaidia katika kuimarisha uchumi wa hao wanaojiweza ili baadae watu wanyanyuke kupitia wao.

Kwanini najaribu kusema serikali nayo imo
1:Wafanyabiashara,wakulima,wafanyakaziwenye viwanda kila mmoja analalamika mzunguko wa fedha umepungua sana. Nani wa kuja na majibu mazuri ya swali hilo kama si serikali, ni nani hapa anayesoma analiyepata briefing kuwa 'tulitoka pale,tupo hapa na tutafika pale'kwa njia hii?

2:A)Malalamiko ya kodi za magari,mitambo na vifaa vingine si mara ya kwanza kulalamikiwa bandarini. Je,serikali imemsaidia nini mwananchi ya kununua gari CIF kwa milioni 5 na kuja kulipishwa kodi pekee ya Mil.6? Mbona hakuna majibu ya kueleweka ya haya maswali?
B)Leo,TRA inakukadiria kodi na hakuna nafasi ya negotiation kati ya TRA na mfanyabiashara mdogo ambaye angetakiwa kulelewa kama mtoto mdogo kama sisi tulivyokuwa tunalelewa nyakati tukiwa wachanga. Hakuna tofauti kati ya uchanga wa biashara na uchanga wa kiumbe hai all need special care.

3: Tunahubiri 'KILIMO NI UTI WA MGONGO KWA WANANCHI WA NCHI HII' Je, migogiro ya wakulima na wafugaji kweli inatatuliwa kwa nia ya dhati kweli kuondoa migogoro hiyo? Kwanini migogoro hiyo inatatuliwa kwa matakwa binafsi ya uongozi, kwanini kusiwe na kipengele cha "kwa mujibu wa kifungu cha sheria no. ____ cha mwaka _____ "

Watakaoinyanyua nchi hii si Wahindi, wala Waarabu, wal wazungu kutoka kona yoyote ya dunia hii. Tuwajali na kuwahudumia kwa haki kulingana na ukubwa biashara yake, capital yake na umri wa biashara yake.

Mwisho nakumbuka mnyukano wa Reginald Mengi na Masilingi wakati ule wa ununuzi wa 'New Africa Hotel"
Mara ikaja watanzania wana fedha za kuwekeza kwenye juice, maneno hayo sidhani kama yanaweza kutolewa na viongozi kutoka kwenye 'developed countries" the phrase "only in Tanzani" halitakoma kamwe. Maana Siri kali imekuwa na wivu na watu wake na watu wake wamekuwa na wivu mbaya wenyewe kw wenyewe. Sijui wa kuionea wivu serikali ni nani, nahisi wanasiasa!

Ngoja tuone kama wazungu wazungu wataijenga nchi hii
 
Back
Top Bottom