Prince Tumbo
JF-Expert Member
- Apr 5, 2013
- 910
- 247
Matukio yanayoendelea nchini kwa baadhi ya watu kutekwa na kuumizwa vibaya yanaaksi nguvu na mbinu
zinazotumiwa na makundi ya kisiasa aidha kwa kulipiza visasi au kudhibiti mipango ambayo inamadhara kwenye maslahi
ya kundi pinzani. Mimi sitajikita kwenye matukio tuliyoyashudia kama kutekwa kwa Dr Ulimboka, kuuwawa kwa
Mwangosi, mauwaji ya Arusha, Morogoro, Ingunga nk. Ninachotaka kukieleza kwa kifupi ni vitisho vinavofanywa
"kimyakimya" na maafisa usalama wa taifa dhidi ya watu baadhi wanaoonekana kutishia usalama wa CCM.
Nimeshapata taarifa kwa marafiki zangu 3 kwa walionisimulia mikasa hiyo walioipata "live" kwa kupigiwa simu na watu
wasiowafamu wakiwaita kukutana nao sehemu fulani tena zenye hadhi kubwa. Japo marafiki zangu hawa waliniambia
haya kwa muda tofauti wote, walikuwa ni viongozi wa CDM kwa wakati huo katika mikoa ulipokuwa wanaishi au
kusoma. Mazingira na nia ya watu waliokuwa wanataka kukutana ni kuwahoji ni kwa nini wanaitumikia CHADEMA.
Hao watatu waliniambia yafuatayo.
Rafiki wa kwanza aliitwa (wakati huo alikuwa mwenyekiti wa CHADEMA tawi la SAUT. Alihojiwa kwa muda wa masaa 3
wakiwa Chistmas hotel (Mwanza). Alitishiwa uhai wake (kama ataendelea kuitumikia chadema) kwamba atakufa na
hapatakuwa na kesi.Mwisho alipewa masaa 10 awe ameshaamua KWENDA CCM au KUACHA SIASA kabisa. Maana
yake ni kwamba alitakiwa mara moja kuacha kufanya siasa akiwa chadema na option aliyopewa ni kujiunga na CCM.
Rafiki yangu kesho yake alijiunga CCM na kwa sasa afisa wa jeshi katika moja ya mikoa ya Tanzania.
Rafiki wa pili na wa tatu (ni wa mikoa tofauti) nao waliitwa kwa staili hiyohiyo na kwa nia hiyohiyo. Mmoja alipewa
saa 9 awe ametangaza au kuacha siasa AU kujiunga na CCM. Yeye kabla ya muda huo aliitwa ikulu ndogo ya
mkoa na kupewa kazi kwa sharti la kuacha siasa kabisa. Wamwisho alijiunga na CCM na kupelekwa kwenye kampeni
za chaguzi ndogo za ubunge na akalazimishwa kutoa ushuhuda kwa kuichafua CDM kama chama cha wachaga, chama
cha udini,nk
My take: CCM kimekuwa kikitumia UWT kutishia watu maisha yao nk, ili wakihame Chama cha Democrasia na Maendeleo. Naamini wapo wengi ambao tayari wameshatishiwa kwa stail hii.
NB;Sikutaka jina la mtu (kati ya marafiki zangu) kwa ajiri ya usalama wao
Karibuni kwa mjadala