Naandika makala hii kuelezea kilio chetu kwa wanafunzi tuliokosa mikopo hususan chuo cha Dar es Salaam Maritime Instutute (DMI). Taasisi hii ambayo inatoa kozi ya Bachelor in Marine Engineering and Bachelor in Marine Transportation, katika mwaka huu imepokea jumla ya wanafunzi 70. Cha kusikitisha katika wanafunzi hao 70 ni wanafunzi wawili tu ndio wamepatiwa loan allocation na bodi ya mkopo na ndio majina yao yamefika chuo.
Swali la kujiuliza, jee ni kweli wanafunzi wawili tu katika chuo kizima ndio wenye sifa? Je, wanafunzi wengine wote waliobaki wakishindwa kujisomesha maana yake ni kwamba kwa mwaka huu DMI itashindwa kusomesha wanafunzi wapya?Malecturer waliokuwepo kusomesha wanafunzi wa Bachelor kwa mwaka huu watakua na kazi gani?
Ushauri:
Naomba bodi ya mikopo ifikirie upya na kwa umakini je hii ni haki chuo kizima kwa mwaka huu kuwapa mikopo wanafunzi wawili tu? Tunaomba bodi ya mikopo, viongozi wa serikali na wadau wa elimu watusaidie kututatulia tatizo hili. Wengi wetu ni maskini na hatuna uwezo wa kujisomesha bila ya mkopo.
Ahsanteni naomba kuwasilisha!