Nature ya kazi zangu imenifanya kuzunguka mikoa mingi hapa nchini, karibia 80%, na hasa vijijini. Nimefanya kazi Lindi na Mtawara about 7 yrs ndo maana nimeizungumzia mazingira magumu waliyonayo wananchi hawa. Kuna vijiji unaenda unaweza kuhesabu nyumba za bati, ukionyeshwa maji ya kunywa hutaweza kuamini kama ni maji ya kunywa mwanadamu. Vijumba vingine milango ni ya makuti tuu na imeegeshwa , habari ya choo ndo usiseme,. Ninakwambia haya kwani nimeshiriki kazi za TASAF 1 kuibua miradi, Miradi ya mazingira n.k kwa hiyo tumezunguka sana kwenye vijiji hivi. Huwezi ukalinganisha Kijiji kilichopo Mtwara au Lindi na vijiji vya mikoa kama Morogoro.