Naomba nikupe ushauli wa tofauti kwa sababu nimeguswa sana, japo Upande wangu sio muoga kama wewe.
Kama upo katikati ya mji hama na mkeo, kapange pembezoni ya mji na ukaanze boda boda maana ni mzoefu katika pikipiki.
Pakia abiria upate pesa ya kula kisha tengeneza mabanda ya kuku wa kienyeji, fuga kuku watano mmoja jogoo mwambie mke awasimamie vizuri.
Endesha bodaboda uku unasoma ramani wapi ufungue banda la chips, na hiyo sehemu utakayo weka banda hakikisha mbeleni unaweza kuongeza supu na chakula.
Tafuta wapemba kaombe kazi bila malipo jifunze, natumaini week moja tu utakuwa umejua kila kitu.
Fanya boda boda jioni saa 12 ingia jikoni tengeneza chips yenye viungo vyote pilipili ukwaju saladi na n.k ukisaidiana na mkeo
Utatoa ajira kwa zaidi ya watu wawili na maisha yatakuwa safi, Utampenda mkeo nae atakupenda, Mwanamke anamtegemea mume kuwa road map so mpe map mwambie ukweli mambo magumu, kama anakupenda mtakuwa wote.
Ukiendelea kuangaika kutafuta suruhu utapoteza time na utalost mpaka pesa ya kunyoa nywele uonekane sio mzima kwenye mabaraza ya wazee shauli yako, nimekupa ushauli kwa sababu njia yako nyepesi sana, sema wewe mzito kufikiri ndio maana huna direction yako.