Hii lodge niliyofikia leo imenikumbusha mwaka 2015 nilipokuwa Arusha field kikazi

TAI DUME

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
8,859
23,119
Hii lodge nikiyofikia Leo imenikumbusha mwaka 2015 nilipokuwa Arusha field kikazi. Naandika huu Uzi nikiwa hapa Musoma (lodge kapuni), sasa hiki chumba kinafanana sana na kile Cha Arusha (Cha Arusha chumba sio mambo yenu yale wazeiya wa kupulizi)

Anyway ilikuwa hivi, enzi zile ujana mwingiii nimefika zangu Arusha nikatafuta pahala pa kujisitiri (namaanisha kulala sio kujisitiri unakowaza wewe bhana).

Mida mida nikatoka zangu kupata msosi wa usiku. Huku na huku nikajikuta nimetimba Shivaz. Enzi hizo inabamba, Malaya kama wote. Mipombe pombe nikaondoka mida mibovu Sana kumbonji.

Kisanga sasa, naamka asubuhi nakuta chumbani yupo demu (ofkoz ni malaya wa pale Shivaz. Khaa, kujikagua nakuta ndom mbili zimetumika. Cha kwanza nikashukuru alafu ndio nikaanza kujishangaa, yani nimechukua Malaya bila taarifa rasmi ya kushirikisha ubongo wangu. Kichwa cha chini cha kingethe thana.

Sasa yule demu alikuwa ameshaoga na kuvaa tayari kwa kuondoka. Unajua kwanini hakuondoka? Mzee nilijuongeza maana funguo nilificha ndani foronya ya mto niliolalia. Kwaio akawa hana jinsi ya kuchomoka. Mana nililala kizembe sana begi la laptop na waleti vipo tuu mezani. Yule manzi alikuwa anapiga ivo vitu kama sio kujiongeza.

Sasa hapo juu nimekwambia nilikuwa safari ya kikazi inabidi niende field vijijini huko. Kwahiyo pia nilikuwa na mzigo wa ofisi kwaajili ya kulipa watu posho zao na ukumbi si unajua Tena maswala ya masemina semina yalivyo. Nilikuwa kama na m7 hivi cash.

Akili yangu ikanituma ile pesa ipo kwenye begi. Kabla sijamsemesha chochote yule nikawahi kucheki kwanza mzigo upo? Kucheki hivi hola. Pesa haipo. Imeyeyuka. Dadeki. Hapa nikajua manzi keshanipiga. Nilipagawa. Fedha ya Ofisi halafu ndio field yangu ya kwanza pale Ofisini na ajira yenyewe ilikuwa mpya. Balaa.

Nikamwambia yule manzi mami ake leo umebugi. Yani umeingia cha kiume. Mzigo utarudisha. Nilomkomalia balaa halafu nishapagawa. Yule manzi aliapia miungu yote unayoijua hadi Budha lakini wapi. Nikamwambia wewe umewapigia simu wenzio mzigo umetolea dirisha. Anambia muulize mlinzi maana chumba changu dirisha lilikuwa linaangalia kwenye kibanda cha mlinzi. Nikamwambia nyie wote dili lenu moja.

Nikampigia simu dereva wa ofisi niliyesafiri nae akaja. Nayeye akapagawa. Mtiti ukawa ntiti. Demu analia mi namkaba shingo. Wahudumu wakaja, meneja akaitwa. Meneja akanijibu simple sana kwamba bro kuna bandiko kila chumba kama pesa au vitu vya thamani vikabidhi kaunta. Yaani muhudumu wa lodge umkabidhi 7m? Tena 2014? Aisee si amasepa na Kijiji? Nikajua huyu meneja nae dili lao moja nikamuunganisha na mlinzi aliyesema hajamuona mtu. Sasa mbona hela haipo? Nikàmbiwa bro labda utakuwa umehonga yote Mana watoto wa kimbulu waliojazana Arusha si mchezo.

Yule dereva niliyekuwa naye alikuwa na ndugu askari polisi pale Arusha. Akaitwa akaja na Difenda. Wakambeba yule dada na kwa kuwa alikuwa upande wetu akabebwa na meneja, muhudumu wa zamu na yule mlinzi, watu wababe sana ilikuwa ni uonevu kwa kweli. Yule polisi akaniuliza tu unauhakika ulikuwa na hela? Ndio. Ok Kama kweli wameiba watasema tu wacha tukawafinye kidogo.

Sasa bhana, wakati tunatoka nao kwenda kuwafinya kuna kitu kikaflash kwenye akili yangu. Nikamwambia wale polisi hold on. Nikatoka nduki kurudi room. Aisee nilipumua kwa nguvu sana, mzigo si nikauona.

Unajua ilikuwaje? Ni kwamba wakati natoka kwenda kula nilijiongeza. Ule mzigo niliuweka kwenye mfuko wa plastic ile mifuko laini halafu nikauficha ndani ya lile sink la maji ya kuflasihia toilet. Yale masink si huwa yanafunguka kwa kule juu. Basi ndio mzigo nikauhifadhi humo maana najijua nilikuwa nikishalewa naweza naweza beba malaya yoyote ambao ni wezi kama wemesomea. Kwahiyo nikaficha huko mzigo kwa usalama. Aisee Nina akili sana si, ndiyo? Yah, mimi sio fala.

Ikabidi nimuite yule bro polisi. Dah jamaa akacheka sana lakini pia alini-mind kimtindo. Ikabidi meneja wa lodge na yule kahaba waitwe room. Aisee yule manzi alinichapa kelbu moja matata sana. Unaijua kelb? Ni lile kofi la nyuma ya kiganja. Huwa linauma sana ukiotewa lakini ni dharau kubwa sana ukichapwa nalo. Ikabidi niwe mpole tu saa utafanyaje hata kama wewe?

Ustaarabu tunauweza waarabu, au sio? Ikabidi kwanza niwapoze. Yule demu nikamtia na 30, meneja nikamtia na 10, yule polisi nikamtia na 50 akawapoze na wenzake wawili alikuja nao. Halafu nikachukua namba ya yule manzi, usiniulize kwanini ila badae akaja kuwa mshikaji wangu sana. Si unajua mamanzi wa Chuga hawanaga kwere.

Baadaye Sasa nakuja kushtuka kumbe muda wote huwa naendesha mtiti niko na boxa tu. Yaani nazulula makoridoni nipo na boxa, khaa aibu sana!

Sasa nipo hapa Musoma muda huu nahofu yale ya Arusha yasije yakajirudia. I love you mai waifu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom