Hii Ligi Yenu Mbona Siielewi?

Hii Ligi Yenu Mbona Siielewi?

reandle

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Posts
11,166
Reaction score
8,159
Basi bwana, baada ya kususa kwenda taifa nikakata shauri la kununua Dish la Azam ili nifuatilie VPL nikiwa home! Let me say this... naipenda zaidi ligi ya nyumbani kuliko hiyo EPL... yaani, ingawaje mie ni shabiki wa Arsenal, kama itatokea, say, kwa upande mmoja Arsenal wanakipiga na Man U/City na upande mwingine Yanga wanakipiga na Azam/Simba na muda ndo huo huo... trust me, nita-opt kuangalia mechi ya Yanga!!

Kwa maajabu, nafunga dishi faster faster... nasubiri kucheki VPL mara ehee, nasikia ligi imesimama!!! Hapo kati kati nilikuwa na mihangahiko ambayo ilinifanya nishindwe kufuatilia kilichokuwa kinaendelea!! Awali, nikahisi ligi imesimama kupisha mechi ya kirafiki kati ya Stars na Swaziland... mara eh, nasiki Maximo na wanawe kajiendea Brazil!

What happened? Nini kimefanya ligi isimame wakati hata mzunguko wa kwanza haujaisha? Wanasubiria katiba mpya, au? Hii ligi mbona ya hovyo hivi? Ina maana Challenge ikapata mwandaaji, ligi isimame tena ndani ya mzungo wa kwanza? Anyway, niache kulalamika inawezekana kuna sababu ya msingi! Can anyone tell me kilichotokea kwenye nchi hii ya maajabu ya kila sekta?
 
ni utararibu tu tuliojiwekea kwasababu mipango yetu si kuundeleza huu mpira bali kupiga pesa at any cost...haijalishi nani anaumia
 
Okwi anataka agombee uongozi wa serikali ya mtaa
 
Ligi ilichelewa kuanza, na kwa utaratibu uliopo, michuano ya CECAFA hufanyika kwenye muda huu ndio maana upangaji wa ratiba ulizangatia hilo hivyo Ligi kusimama baada ya raundi saba.
 
Ligi ilichelewa kuanza, na kwa utaratibu uliopo, michuano ya CECAFA hufanyika kwenye muda huu ndio maana upangaji wa ratiba ulizangatia hilo hivyo Ligi kusimama baada ya raundi saba.


Long time Lonestriker sijasoma comment zako. Nimefurahi kuona uwepo wako
 
Back
Top Bottom