Hii kauli "Simba dhaifu" inatugharimu sana Yanga

Mada za hivi ndizo zinapaswa kuwepo jukwaani
Ukweli ni kwamba Simba ni timu yenye uwezo mkubwa tu dharau za baadhi ya wanayanga ni upungufu wa hekima au ushahidi kuwa watz wengi vichaa
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Hizi kauli ni zetu mashabiki mkuu sio za wachezaji na benchi la ufundi.

Ni sawa na ile Pacome day, watu walisema tumewekeza kwenye PDay badala ya kujiandaa, mwishowe mtu akala 4.
 
Nikiri wazi mimi ni shabiki kindakindaki wa timu ya Yanga.

Katka zama za hivi karibuni imeibuka misemo kwa sisi wana Yanga kuiona Simba ni dhaifu na sisi ni bora zaidi.
Ukiangalia mechi anazocheza Simba na timu anazokutana nazo matokeo ni tofauti kabisa na kauli ya Simba dhaifu.

Ni wazi zile 5 tulizowafunga ndio zinatupeleka kuona Simba dhaifu kwa kutumia hesabu zetu za algebra. Kwa mfano ikitokea Simba imecheza na timu nyingine halafu wakstoka sare, hesabu zetu zinakua kwa kuwa Simba katoa sare na hii timu na kwa kuwa sisi tuliifunga Simba, basi hata hawa tutawafunga. Tukiingia uwanjani na hiyo timu ni aidha sare au tufungwe(rejea mechi na ahly).

Sasa kwa kigezo hicho ubora wetu upo wapi na udhaifu wa Simba upo wapi wakati wanapata matokeo na wanasonga mbele. Timu dhaifu tupo nayo Robo fainali.

Sasa hivi tunaomba eti tukutane na ASEC kwa kuwa katoa sare na Simba tunaona tutawaweza. Niwakumbushe tu mashabiki wenzamgu wa Yanga, hao ASEC waliotoa sare na Simba tukipangwa nao sisi tutapigwa. Kwa sababu tutaingia na mentally ya sisi ni bora, tukifika uwanjani mambo tofauti.

Ifike wakati zile 5 isiwe kigezo cha kutambua ubora wetu. Hata wale galaxy tuki cheza nao kesho tunaweza kupigwa au kutoa nao sare. Kwa nini, kwa sababu ya hesabu zetu za algebra kwa kuwa simba kashinda 6 na sisi tuliwafunga simba 5, basi tutawafunga galaxy 30.

Tunapoingia uwanjani na timu yoyote tusiwe na akili za hawa tutawapiga ni wepesi. Hii inatugharimu sana. Tuingie uwanjani kwa falsafa ya vita kufa au kupona. Yule msemaji wetu kiukweli nae anachangia katika kusababisha timu kufungwa kwa sababu kuna mentality anaiweka kwa wa chezaji na mashabiki kabla ya mechi. Hii ni suala la sailolojia asije mtu kusema kwani msemaji anacheza namba ngapi uwanjani. Tusiwadharau wapinzani wetu.

Nawasilisha.
Hoja yako ni msingi sana kuhusu kutomdhara Opponent yeyote, lakin hoja yako haibadili maana ya Simba kudhoofika kiwango hivi sasa
 
Itoshe Tu kusema wewe ni TAAHIRA...
Ihefu aliifunga Yanga baadae alipigwa karibia game tano mfulululizo ...
Usitusingizie Wanayanga Sisi tunauheshimu mpira Simba kabla ya kumpiga 5 alitupiga mbili bila kama hesabu zako hizo zingekua sahihi basi tusingemfunga...
Wewe n kolo mtakatifu
 
Ntia maada jijibu mwenyewe, kati ya wale wapinzani wa Yanga robo fainali nani ana afadhali kidogo?
 
Back
Top Bottom