Hii inawahusu wanawake wa mikoani hasa mabinti

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,540
7,452
Kituo cha Mabasi Ubungo chageuzwa Kambi ya Mabinti wanaotelekezwa na Wenyeji



Abiria-wakiwa-katika-Stendi-ya-Mabasi-yaendayo-mikoana-nchi-jirani-750x350.jpg

KITUO Kikuu cha Mabasi Ubungo, Dar es Salaam, kimegeuzwa kuwa kambi ya mabinti wanaotelekezwa na wenyeji wao, baada ya kuitwa kutoka mikoani kwa kutumiwa nauli, lakini wanapofika kituoni hapo huwakosa wenyeji wao na kuamua kuweka kambi eneo hilo.

Mabinti hao, maarufu kwa jina la ‘vipaseli’ kama wanavyojulikana katika kituo hicho kikuu cha mabasi ya abiria, baadhi yao wanadaiwa kuitwa na baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanaohitaji wasaidizi wa shughuli za ndani, huku wengine wakidaiwa kuitwa na wanaume wenye tabia za ukora.

Inaelezwa kwamba wengi wa wanaume hao, huwasiliana kwa njia ya simu na mabinti hao na kufikia makubaliano ya kuwasafirisha hadi Dar es Salaam kwa kuwalipia nauli ambayo mabinti hao hutumiwa wakiwa bado makwao na kuelekezwa washuke ndani ya kituo hicho ili wapokelewe na wenyeji wao.

Hata hivyo, inaelezwa kwamba mabinti hao wanapowasili kituoni hapo, wenyeji wao hao huingia mitini, kwa kutofika kuwapokea hali inayowalazimu mabinti hao ambao baadhi yao wana umri wa chini ya miaka 10, kukosa mahali pa kwenda na kuamua kuweka kambi katika eneo hilo.

Jengo-la-kupumnzikia-abiria-wanotoka-katika-maeneo-mbalimbali-nchini-na-nchi-jiranipsd.jpg


Jengo la kupumnzikia abiria wanotoka katika maeneo mbalimbali nchini na nchi jirani

Uchunguzi uliofanywa na FikraPevu umebaini kwamba mabinti hao wameamua kuishi maisha ya kuuza miili yao kwa vijana wanaofanya kazi za kubeba mizigo kituoni hapo pamoja na wahudumu wa mabasi hayo yaendayo mikoani.

Katika uchunguzi wetu huo, imebainika kwamba wengi wa mabinti wanaotelekezwa kwa kukimbiwa na wanaume waliowaita, hua wanakosa vigezo ambavyo wanaume hao walivitarajia.

Kwa mujibu wa uchunguzi wetu huo, wengi wa mabinti hao hutoka katika mikoa ya Iringa, Kagera, Njombe, Mtwara, Lindi, Shinyanga, Arusha na Mwanza.

Mmoja wa mabinti hao aliyekubali kuzungumza na FikraPevu ni Sauda aliyekataa kujitambulisha kwa jina la mzazi wake, lakini akisema ana umri wa miaka 25.

Katika simulizi yake, Sauda anasema alianza kufahamiana na mwanaume aliyemshawishi kuja Dar es Salaam, kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, kupitia simu yake ya mkononi.

Sauda ambaye ni mwenyeji wa Lindi, anasema mwanaume huyo baada ya kuwa na mawasiliano (chat) ya siku nyingi, alimuomba aende Dar es Salaam ili waweze kukutana ana kwa ana, kwa ahadi ya kuanza mahusiano ya kimwili au uchumba.

“Tulikuwa tuna-chati mara nyingi tu usiku kwenye Facebook, kila mmoja akisema amempenda mwenzake. Akaniuliza kama niko tayari kuja Dar es Salaam, nami nikamwambia hakuna shida yoyote kama atanitumia nauli,” anasimulia Saunda na kuongeza.

Baadhi-ya-abiria-wakiwa-katika-jengo-la-kupumnzikia-abiria-wanotoka-katiak-maeneo-mablimbali-nchini.jpg


Baadhi ya abiria wakiwa katika jengo la kupumnzikia abiria wanotoka katika maeneo mbalimbali nchini na nchi jirani wakiwa wamepumnzika ndani ya jengo hilo

“Siku ya siku akatuma kweli nauli (kwa kutumia huduma ya fedha ya simu za mkononi). Nikawaaga nyumbani na njiani tukawa tunawasiliana na wakati mwingine kuchati kwa ujumbe mfupi wa maandishi hadi nikaingia Dar es Salaam.

“Lakini nilipofika Dar es Salaam, sikumwona. Aliniambia nitoke nje ya kituo, nikae nje ya mlango wa kuingilia nimsubiri hapo anakuja kunichukua na gari.

”Ilikuwa ni jioni kama saa 11 hivi, lakini nilikaa hapo hadi saa tatu usiku, kila nikimpigia simu akawa hapokei, nikimwandikia meseji akawa hajibu, nikaamua kulala hapo hapo nje hadi asubuhi…hapo nikajua nimetapeliwa.

“Sikuwa na nauli ya kunirudisha nyumbani kwetu Lindi, nikaanza kuhangaika kutafuta kazi yoyote ya kufanya ili nipate fedha kwa ajili ya matumizi, nikawa sipati kazi yoyote ya maana.

Baadhi-ya-abiria-wakiwa-katika-jengo-la-kupumnzikia-abiria-jijini-humo.jpg


Baadhi ya abiria wakiwa katika jengo la kupumnzikia abiria Jijini humo

”Nikaanza urafiki na mdada mmoja wa umri wa kati ambaye mara kwa mara anakuja kituoni hapa usiku. Akaniambia niende naye tukafanye kazi na yeye atakuwa mwenyeji wangu.

”Nilipomuuliza mdada yule ni kazi gani hiyo, hakuniambia ni kazi gani, akasema ni ya kawaida lakini nitakuwa naifanya usiku tu.
”Awali nilimkatalia na baada ya kuulizia zaidi niakaambiwa na mambinti wengine anaokuwa nao, wakaniambia alitaka kunipeleka kwenye sehemu za starehe, kwenda kuuza miili.”

Baadhi ya wakazi wa eneo linalozunguka kituo hicho cha Ubungo wameiomba Serikali, kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, kutafuta namna ya kuwasaidia mabinti hao kuwarejesha makwao kabla hawajaathirika zaidi kutokana na aina ya maisha wanayoishi kkatika kambi yao hiyo. Juhudi za kuwasiliana na mamlaka hizo ili pamoja na mambo mengine waweze kuzungumzia namna ya kuwasaidia mabinti hao, zinaendelea.
 
Eti anawasiliana na mtu Facebook mpaka unakuja dar!!! Shukuru Mungu haujabakwa bali umeamua kufanya umalaya wako
 
Na baada ya kufanya huo umalaya si qmeshapata nauli mbona harudi kwao kama sio malaya ni nini?
 
Hizi ndiyo changamoto za utandawazi, kikubwa mabinti wasipende vya mteremko katika maisha kwani gharama yake ni kubwa sana, chukulia unachat na mtu mwisho wa siku eti safari kumfuata huko, sasa ukifika unakuwa mtumwa wake, kama ana matatizo ( afya, nk) moja kwa moja nawe unayapata make unakuwa huna namna.
 
Inabidi sasa waombe kutumiwa nauli ya kwenda na kurudi plus lunch na vocha.....kama vipi na ya geati kabisaaa in case hatoonekana wadada wapate pa kulala

Maana kuwashauri waache mahusiano ya mtandaoni hawasikii
 
Imezoeleka wamama ndo hutuma nauli ili kupata mabinti wa kazi. Eh kumbe hadi wanaume nao hutuma nauli ila kwa lengo lingine. Mhhh
 
Hawa wanaume sio kwamba hawafiki, wanafika na kukaa pembeni wakisha ona kitu chini nyembamba juu nene hatua inayofuata ni kulala mbele.
 
Back
Top Bottom