Thanx alot keep it up
Habari wana jf.
Kumekua na mkanganyiko sana katika lugha tunazotumia wana jf hasa kuhusiana na watu wenye ulemavu. Kwa kutumia taaluma yangu nimeona bora nitoe darasa na yeyote mwenye swali au maoni awe huru kuuliza. Ni ufafanuzi wa majina sahihi ya watu wenye ulemavu
1. Albino
Huyu ni mtu mwenye ulemavu wa ngozi na anatambulika sana kwa muonekano tu. Tafadhali usimuite ZERUZERU, dili, mzungu au majina mengine yanayodhalilisha utu wake. Jina sahihi ni albino au mwenye ulemavu wa ngozi.
2. Kiziwi
Huyu ni mtu mwenye upungufu wa usikivu either hasikii kabisa au ana usikivu kidogo (residual hearing). Hawa wanatambulika hasa kwa kutembea makundi makundi na wanatumia lugha ya alama (nyie mnaita lugha ya ishara au mikono). Ni mara chache sana kumkuta kiziwi anatembea peke ake .Usimuite BUBU au ASIYESIKIA (huyu ni kiburi). Tafadhali muite kiziwi ndo jina lenye heshima kwake.( nahitaji maswali mengi sana kuhusu kundi hili maana nalifahamu kuliko makundi yote hapa).
3. Asiyeona
Usithubutu kumuita KIPOFU maana kipofu ni mjinga wa jambo fulani ndo mana tuna vipofu wa mapenzi nk. Muite asiyeona tu lina heshima na hadhi na hawa wanatambulika sana kwa fimbo nyeupe maalum wanayotumia kutembelea au wanakua na muongozaji.
4. Mwenye ulemavu wa akili
Usimuite taahira, ndondocha, au chizi. Hakupenda kuwa ivo ila jina sahihi ni mwenye ulemavu wa akili na hawa wako makundi tofauti kama wale wenye autisim na mental retardation ni watu wawili tofauti japo wote ni wenye ulemavu wa akili.
N.B. Kuna aina nyingi sana za ulemavu siwezi kuzianisha hapa ila tuwe waangalifu kwa majina tunayotumia kuwaita hawa wenzetu wenye ulemavu manake wenyewe wanasema kila mtu ni mlemavu mtarajiwa so take care. Nakaribisha maswali na maoni
Naomba kuchangia kulingana na uwelewa wangu. Hawa walemavu wanamajina ya utambulisho kama vile kiziwi, kipofu, bubu, zeruzeru nk.
Kumwita mtu kwa kutumia kiwakilishi (ki) ni kumfananisha na kitu kama vile, Kisu, kijiko, kiti, kikombe nk. Lugha nzuri ya kutumia kwa hawa ndugu zetu iwe hivi:
1. Kipofu= Asiyeona
2. Kiziwi= Asiyesikia
3. Zeruzeru = Albino
4. Kwa walemavu wa miguu au mikono kuna watu wanawaita vi(ki)wete. Neno sahihi hapa ni mlemavu.
5. Kichaa, mwenda wazimu, chizi huu si ulemavu huu ni ugonjwa that why wanapatiwa matibabu. Hawa wanaitwa wagonjwa wa akili.
Ahsanteni
mheshimiwa, wewe unaleta political correctness. usinielewe vibaya lakini
1.kipofu- kiswahili fasaha ni mtu asieona,hamna ubaya wowote kutumia hili jina kwa maana yake halisi.
2.kiziwi-kiswahili fasaha ni mtu asiesikia,hamna ubaya wowote kutumia hili jina inavyotakiwa.
mimi natoa elimu ili msijikute mmeingia kwenye matatizo yasiyo ya msingi. Hebu kutana na prof bagandashwa ni asiyeona yupo pale udsm afu muite we kipofu uone atakavyo react. Au asiyeona yeyote jifanye hujui tu muite kipofu unless awe hajitambui kama wale wanaowekaga vikopo barabarani na kuomba omba
Range of deafness
Mild deafness - people who are
hard of hearing may have a little
difficulty following speech in
certain circumstances, especially if
there is a lot of background noise,
but can generally cope if the
environment is favourable.
Moderate deafness - people with
moderate deafness have some
difficulty in following speech in
most settings, but can generally get
a lot of help from wearing a
hearing aid.
Severe deafness - people with
severe deafness hear no speech
without the help of a hearing aid.
Profound deafness - people who
are profoundly deaf hear no
speech, even with the benefit of a
hearing aid( hope mmeamini sasa kuwa kiziwi sio lazma awe hasikii kabisa)
Mtoa mada.
Unaleta kitu inaitwa ubinadamu na sio ufasaha wa lugha.
Hayo maneno yote yapo kama ulivyoyapinga.
Naungana na RRONDO
Usituelewe vibaya.
Aisee bagandashwa nilimwandikia makala miaka mingi. Naomba mawasiliano yake. Wakati huo aliishi ubungo kibangu nadhani.