Hii inafaa kweli? Njooni tutoe mitazamo yetu

Hii inafaa kweli? Njooni tutoe mitazamo yetu

Mr Leo

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2021
Posts
602
Reaction score
1,271
Habari za muda huu wanajamvi?

Natumaini wote ambao kwamba tumeafikishwa kupitia uzi huu mwenyezi mungu ametujaalia umri na afya njema na hili pia ni katika majambo ya kushukuru kila siku.

Moja kwa moja niende kwenye jambo ambalo nimekuiteni hapa wanajamvi tutoe mitazamo yetu kila mmoja..

Kuna watu kuzungumza, naomba nijaribu kufaisiri maana ya mazungumzo au watu kuzungumza kwa kadiri nielewavyo Mimi

Watu kuzungumza hii inamaana ya watu kuongea kwa lugha nzuri zilizo na maadili ndani yake na staha na Kueleweshana kihoja, huyu anatoa hoja yake na dalili zake kadhalika yule anatoa hoja zake na dalili zake pasi na pande yeyote kumlazimisha mtu kuwa pande yake ndio ipo sawa ila hoja zenyewe zinakuwa zinajieleza utang'amua mwenyewe kwa muda na wakati wako

Na kuna watu kujadiliana, hii pia nitaomba nijitahidi kuhifasiri kwa nijuavyo Mimi

Kujadiliana kwa maana ya mjadala hii ni kama hiyo ya kwanza (mazungumzo) ila huwa ina features zinaongezeka kama vile ubishi, kukosekana kwa lugha ya staha tena, mtu kuvutia upande wake bila hata kuwa na hoja na muda mwingine ugomvi na chuki na uhasama uzaliwa kabisa hapa

Na tatu kuna watu kuanza direct kwa kutukana na kutumia lugha chafu bila hoja na matusi juu, hii nimeshindwa hata niiweke kundi gani

Hoja yangu ilikuwa ni hii

Humu jf huwa kuna threads nzuri sana zinaanzishwa zinakuwa na maswali fikirishi na zinakuwa zina maswali ambao wengi tunatamani tupate majibu tuna tamani tuwe na mazungumzo mazuri kwa njia yetu hii pendwa ya keyboards tupate majibu na maono tofauti tofauti

Lakini kwa bahati mbaya mkiwa kati kati ya mazungumzo au mwanzo tu wa mazungumzo yenu atatokea mtu atatumia maneno machafu juu pande nyingine hata baadhi ya watu wenye madini na kujiheshimu anaona haya kuangusha wino wake kwenye sehemu ambayo ushakuwa chafu tayari kwa maneno machafu yaliyoandikwa mwisho wa siku uzi unakufa na kukosa majibu isipokuwa watu kutukana kwasababu ya kutumia fake ID

Sio kwamba sipendi critics, hapana, nazipenda haswa! Sema nazipenda critics za hoja na sio matusi maana critics zinajenga na zinamfanya mtu asome zaidi juu ya jambo hilo, ila wengi sikuhizi humu jf watu hawaleti critics (arguments) Bali ni matusi amabyo mengine ukisoma tu unatoka kwenye uzi hapo hapo

Je, imekaa vipi kama ingelikuwa na uwezo kwa alieanzisha thread kuwa na uwezo wa kumtoa kwa thread mtu ambae anatabia kama hizo chafu za kutokuleta arguments kwenye mada flani Bali matusi machafu na mengineyo ili thread iweze kuishi na kufaidisha wengiene?? Maana mods wanajitahidi kuwapiga ban hawa watu wenye maudhui machafu ila bado hawajafanikiwa kwa kiasi kizuri

Weaknesses: kama muanzisha thread atakuwa na hiyo control access ya kufanya hivyo basi kuna muda anaweza asiwe muadilifu kwa sababu tu hampendi member flani basi hatotaka ashiriki kwenye nyuzi zake

Karibuni na mitazamo yenu wakuu
 
Sometimes mada inakuwa nzuri kwelikweli ila anakuja mtu anawatoa kwenye reli unaona ni upuuzi tena uzi wenyewe
 
Na wengi sjui ni depressions ndio sababu maana mtu mwenye akili timamu si mwepesi kuwa mtu wa kutamka matusi
 
Back
Top Bottom