Hii ina faa sana

mdesi

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2013
Posts
1,375
Reaction score
2,267
Ndugu wana jf, hapa napenda kuwashirikisha njia za kutoa vitambi kabisa/kutopata kitambi. unaweza fanya mojawapo au zaidi kati ya haya

1.Uwe na mikopo zaidi ya mmoja katika benki tofauti inayozidi uwezo wa kuilipa. ie uwe unashindwa kulipa kwa wakati.

2. Kama bado hujaoa, basi oa binti wa miaka 18 hivi awe wa kuvutia sana.

3. Kama unaishi dar jitahidi uwe na watoto wengi huku ukiishi vyumba/chumba cha kupanga. Na mke awe ni mama wa nyumbani. ie. familia iwe inakutegemea wewe tu.

4. Kama umejaliwa kuwa na pesa hasa ya biashara basi ingiza mtaji wako kwenye malori tu.

5. Kama unataka kuajiriwa jitahidi uishi kibamba afu kazi ufanyie posta. repoting time saa moja na nusu exit saa 11 jiomi(private co.)
na mshahara usizidi 250,000 kwa mwezi.

Haya ni machache yanayoweza kusaidia kumaliza vitambi vyote au kuto kuwepo nacho kabisa. Karibuni wana jf kuongezea km zipo myimgine.
 
Kitakachofuata apo ni presha na sio kupunguza kitambi tena.
 

hatuchangii chochote, sababu: "no research no right to speak- kubwabwaja"
 
Ishi mabondeni kipindi cha mvua

Uwe kocha wa simba au yanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…