Hii imekaaje?

Anfaal

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2010
Posts
1,154
Reaction score
118
Nakumbuka zama hizo (sina hakika na sasa) ukiingia kwenye nyumba ya mtu Unakutana na maandishi " mgeni karibu nyumbani uyaonayo na kuyasikiayo hapa yaishie hapahapa". Hii ni karibu kweli? Hivi maandishi haya yanamanufaa yoyote? Pamoja na maswali hayo hebu tujikumbushe maandishi ambayo hukutana nayo katika nyumba zetu.
 
Nyumba yangu ni ndogo, haina nafasi ya kuweka fedha wala dhahabu ila upendo.
Cha kushangaza hata kwenye mahekalu ya mafisadi wanatundika poster kama hizi.
 
Maneno mengine huwa yanaleta maana mbaya sana, lkn watu wanayatundika tu! Na hii mara nyingi huonyesha tabia ya mama mwenye nyumba hiyo
 
Nyumba hii inalindwa na ......... (kama inalindwa kuna haja ya kuandika hayo yote???)
 
Binafsi naona huo ni urembo,na urembo unamanufaa kwa yule autumiae,kwahiyo yeye aloweka urembo huo lazima unamanufaa kwakwe na ww kama ujumbe huo utakugusa basi ni mesage sent.
 
heee utasema maneno ya kwenye kanga? Huh Huh
 
Binafsi naona huo ni urembo,na urembo unamanufaa kwa yule autumiae,kwahiyo yeye aloweka urembo huo lazima unamanufaa kwakwe na ww kama ujumbe huo utakugusa basi ni mesage sent.

Maneno yamebandikwa sebuleni iwe msg sent kwangu??? No pls! Binafsi naona ni ushamba na ndio maana nimesema enzi hizo.
 
Haya maandishi yanafanana na wale wanaobandika certificates zao sebuleni!!!!! Arrghhh!
 
hahaha anfaal ....................mie nikienda kwenye nyumba nikakuta certificate zimetiwa frame zimetundikwa ukumbini huwa naona 'raha' kweli πŸ˜€
 
hahaha anfaal ....................mie nikienda kwenye nyumba nikakuta certificate zimetiwa frame zimetundikwa ukumbini huwa naona 'raha' kweli πŸ˜€

Gaijin, hebu imagine unaanza unabandika ya wewe na kama una partner na yeye anabandika, km unawatoto wanabandika ohpss. Ah ni bora basi watengeneza album ili akifika mgeni wanamuonyesha ya picha then ya certificate. Ukutani inakuwa kama makorokoro. Enzi zile vijana walikuwa wanabandika magazeti kwenye maghetto yao. Wengine picha za wachezaji wa Simba na Yanga etc. Mh lakini ni mtazamo labda ndio inatakiwa hivyo!!!
 
pata picha .....watoto watano wote wana angalau masters .................lazima kuta za nyumba zigeuke kama museum πŸ™‚


lakini inaonyesha tu mapenzi na furaha ya mzazi kwa mwanawe kufikia mafanikio hayo na hasa mara nyingi ikiwa mzazi mwenyewe mafanikio hayo hakuyapata.

lazima u-brag kama mwanao daktari ati πŸ™‚
 
sioni ubaya, nadhani ni ujumbe tu wa mgeni kuzingatia.
 
Achana na enzi hizo hata siku hizi bado watu wanabandika matangazo au hayo maandishi sebuleni na kusudi ni kuwa kila aingiaye atasoma na ujumbe utakuwa umekufikia. Tofauti inakuja siku hizi watu wako kisasa zaidi wanabadika au ujumbe kwa njia ya picha au maandishi na picha.

Hivyo wewe msomaji kama utafurahia ni sawa tu na kama utona ni ushamba ni sawa tu lakini mbandikaji ndo kabandika.

Labda kwa kuongeza ingawa ni kwa asilimia ndogo au nusu ujumbe wowote unaobandikwa sebuleni hutoa picha ya tabia ya mmiliki wa hiyo nyumba, maana jumbe zingine ukiziona moja kwa moja unahisi kuwa wenye nyumba hii ni washirikina, wacha Mungu, n.k wa kadhaa.

ni mtazamo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…