Hakuna kuogopana, kama utaugopa huwezi kuleta mabadiliko, ni watu jasiri tu ndio huleta mabadiliko na wakati mwingine sio kwa faida yao. Hapa jamii kuna majukwaa mengi mbali na hili jukwaa la siasa, kuna wengine ni wataalam wa masuala ya ujasiria mali lakini hawana mtaji kuna wengine wana mtaji lakini hawana elimu ya ujasiriamali, jamii forums inaweza kuleta mabadiliko mbalimbali yanayoshikika. Huwezi kuleta mabadiliko kwa kujifungia ndani hata kama unawazo mazuri. Hakuna jambo zuri lisilo na changa moto.