​Wana JF,
Naomba msaada wa wataalam wa picha na TV.
Kuna kitu kwenye picha kinaitwa "aspect ratio", hii ni ratio ya urefu na upana wa picha ili picha ionekane katika uhalisia wake.Katika TV za kizamani (mitungi) hili linadhihirika na picha iliyorushwa inaonekana katika uhalisia wake, lakini katika TV za kisasa (flat screen) picha inaonekana bapa, yaani urefu unapungua na upana unazidi. Hii imenifanya nisinunue flat screen na siku zote natumia mtungi.
Naomba mnijuze kwamba flat screen ndivyo zilivyo au ninaweza kupata iliyo na ratio sahihi?
Unaweza ku-adjust kwny TV yako ikawa size yeyote utakayo. Depends on your flat screen (if its SONY, Samsung etc) but generally follow:
Adjust your aspect ratio - Get the best picture from your flat-panel display - Weekend Project - CNET Reviews
Aspect ratio (image) - Wikipedia, the free encyclopedia
Widescreen-o-Rama! All About Aspect Ratios
Ahsante sana kwa hiyo shule, ngoja nitayaona.Pia ni muhimu kufahamu chanzo (source) ya midia unayotaka kutazama. Mf. Filamu (naamanisha filamu sio video) nyingi zinakuwa na aspect ratio ya 16:9, wakati matangazo ya TV hapa kwetu bado yapo katika 4:3
Sawa utafanya yote lakini ukweli utabaki palepale, ubora wa picha ama video ya tube tv uko juu kuzidi LCD tv, mi hata niwe na mamilioni siwezi nunua flat tv ie LCD, zoezi dogo chukua old sony wega flatron linganisha na hii misony yao mipya utakubaliana na mimi, ukizingatia wengi wanatumia av cable kusafirisha picha kutoka vyanzo kama VHS na DVD PLAYER. ukitumia HDMI cable angalau kidogo ubora unakaribiana. ndio LCD zinamanage space lakini very delicate. nashauri ni bora ununue king'amuzi uunge tube tv.
​Wana JF,
Naomba msaada wa wataalam wa picha na TV.
Kuna kitu kwenye picha kinaitwa "aspect ratio", hii ni ratio ya urefu na upana wa picha ili picha ionekane katika uhalisia wake.Katika TV za kizamani (mitungi) hili linadhihirika na picha iliyorushwa inaonekana katika uhalisia wake, lakini katika TV za kisasa (flat screen) picha inaonekana bapa, yaani urefu unapungua na upana unazidi. Hii imenifanya nisinunue flat screen na siku zote natumia mtungi.
Naomba mnijuze kwamba flat screen ndivyo zilivyo au ninaweza kupata iliyo na ratio sahihi?
Nashukuru mkuu, ngoja nitaifanyia kazi ni enjoy mavituz ya kisasa.