Hii imekaaje jamani

KASINYE

Member
Joined
Jun 6, 2014
Posts
85
Reaction score
24
Binti alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mme wa mtu, penzi limenoga kiasi cha kila mmoja wao kufahamu mambo ya mwenzake kiundani, mke wa jamaa akafahamu mchezo akampandia yule dada, dada wa watu akaona imekaa vibaya akamuomba jamaa waachane asimwalibie ndoa yake, jamaa akagoma yakabaki mapenzi ya wizi.

Siku moja dada huyu akawa na shida ya fedha na mshahara haujatoka jamaa akamwambia atampa hicho kiasi cha fedha lakini aendapo safari amwachie kadi ya benki, kwavile waliaminiana hakukataa akampa kadi hiyo.

Dada amesafiri mshahara ulipotoka jamaa akatumiwa password akachukue pesa awalipe baadhi ya watu waliokuwa wakimdai dada huyu na kiasi kingine amtumie, amerudi toka safari akamweleza jamaa amepata mchumba na yeye anahitaji kutulia na mme wake.

Jamaa kuambiwa hivo akakatalia kadi ya benki demu kakomaa na msimamo wa kuachana naye na kumweleza kama kuna kitu alimnunulia kinamuuma akachukue, kweli jana jamaa kaenda kubeba TV aliyokuwa kamnunulia demu bado kadi hataki kurudisha, demu kakomaa jamaa kaenda kukomba mshahara wa dada huyu wote na masalia yake akamwamwichia 50 elfu.

Dada wa watu analia tu anatakiwa awalipie ada wadogo zake, jamaa anasema eti atamtafuta tu.

Wadau ni kwanini tusikubaliane na matokea tunapokataliwa na ukizingatia jamaa ameoa? eti hoo! tuliahidiana kuzaa naye!!!!!
 
Akamwambie mkewe amchonganishe mpaka waachana.ubaya kwa ubAya
 
Hayo ndiyo maalipo ya kuingilia ndoa za watu.
Shaur yake
 
Huyo jamaa anaeiba hela za mwanamke ni kapuku tu....
 
Hii ndo hatari ya kucheza na hisia za watu.....ahame mji.....
 
hiii imekaeje????

jamaa maskini tuuuu
 
kinachotakiwa bint aende kwa mkewe,amweleleze ukweli kama mke mwelewa atamsamehe then wakae na mumewe akigoma bint aende bank aombe form ajaze faster abadili namba ya sir fasta,huku akisubiri kadi yake kwa jamaa loo kazidi nae mume wa mtu unamwachia kad aende kutoa mahela unalo sasa utaliona la moto mwanamke akili yako iko wapi ww???
 
kweli na atangaze kwa mkewe loo
mke wa jamaa alishamkanya huyu dada mpaka akaripoti ofisini kwao lakin huyu dada alikuwa kakomalia tu, nahic akifaham nahisi atashangilia badala ya kumchanjia mmewe
 
hiii imekaeje????jamaa maskini tuuuu
Jamaa ni mtumishi na ana miliki magari 2 mimi naona anataka demu akubali kurudiana naye ndo kisa cha kumpola pesa hiyo kwa kujua ata haso amrudie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…