Konakali
JF-Expert Member
- Dec 15, 2009
- 1,533
- 263
Katikati ya mwaka 2006, ulikuwa mahali fulani ukifanya field yako ya kumalizia chuo kwa miezi sita (6) katika taasisi moja. Ukiwa completely single, ulipanga katika nyumba moja ambayo pia alikuwepo mdada mmoja naye kapanga akifanya kazi katika taasisi nyingine tofauti na ile uliopo wewe. Mdada huyu alionesha kila hali ya kukupenda na kutaka ushirikiano wako mara nyingi, kama sio zote. She is very charming to you, and very corparative. Then ukaamua kujibu hisia zake kwa namna ya kuitikia, lakini akaweka msimamo kuwa hawezi kufanya mapenzi hadi mkajitambulishe kwa wazazi, kitu ambacho kilikuwa si rahisi kwa kuwa hujamfahamu vizuri na unabanwa pia na shule yako, hata kifedha ukawa hujajipanga vya kutosha kwa hilo, kadhalika yeye mwenyewe alionesha kutokuwa tayari akidai ni mapema mno. Ila kila aina nyingine ya company uliyohitaji ulipewa. Mwanzoni mwa mwaka 2007, mdada huyo aliweza kupata kazi mkoa mwingine ambapo aliondoka na alikuaga, na akiwa huko mliendelea kuwasiliana kama miezi sita tena, ambapo alikuaga kwa simu kuwa anakwenda Ulaya kusoma. Huko mawasiliano yalipotea kabisa, na kwa kuwa pia hukupewa ahadi ya kwamba mambo yatakuaje atakaporudi, August, 2008 ulikutana na binti mwingine ambaye naye alionesha kukuhitaji katika maisha yeke, engagement ilanza baada ya muda na baadaye mkaoana June, 2009 na baada ya muda mfupi mkajaliwa mtoto. Mnamo March, 2010, ghafla uliipata "missed call", na kwa kuwa ulipata kupotezapoteza simu, namba hizi zilionekana kuwa ngeni kwako, lakini ulipiga na kuulizia "nani mwenzangu". Ukakutana na sauti yake akikujulisha kuwa amekwisharudi toka Ulaya na sasa yupo tayari kwa ulichokitaka. Msimamo wako ni kwamba haupo tayari kumkosea wala kumpoteza mkeo wa sasa. Pia usingependa kumuumiza mdada huyu, lakini ukweli wa mambo aupate. Ila tangu mlipoanza kuwasiliana tena hadi sasa hamjawahi kukutana ana kwa ana, pengine ungewezapata kumweelewesha.
SWALI: Utafanya nini ili huyu mdada apate ukweli, tena bila kuumia wala kukulaumu, na pia bila wewe kutia doa kwenye ndoa yako?
SWALI: Utafanya nini ili huyu mdada apate ukweli, tena bila kuumia wala kukulaumu, na pia bila wewe kutia doa kwenye ndoa yako?