Hii hapa ndoa yako imara na yenye mafanikio

Hii hapa ndoa yako imara na yenye mafanikio

b191

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
742
Reaction score
1,032
Habari za muda huu wadau wa JF,

Leo napenda nitoe somo kidogo juu ya namna ya kufanya Ndoa yako iwe imara na yenye mafanikio.

Somo hili litatuhusu sote, tulio kwenye Ndoa na tusio kwenye Ndoa.

Ukiwa kwenye Ndoa zingatia mambo haya;

1. Kutengeneza fomula mpya ya maisha, Mwanaume au Mwanamke anapokuwa kwao au kwake huwa na fomula yake ya maisha. Sasa ili kufanikiwa katika maisha ni kazima nyote wawili mkae pamoja na mtengeneze fomula mpya ya maisha. Fomula mtakayo tengeneza itawasaidia sana katika maisha yenu ya Ndoa kwa sababu mtafanya kile mlichokubaliana.

2. Msiige maisha au fomula ya mtu mwingine. Hapa watu wengi huwa tunakosea kwa kuiga fomula za watu wengine. Kumbuka maisha ya Ndoa hayana fomula maalumu.
Mfano 1+1 kwa mwenzako inaweza kuwa ni 2 lakini ukiiga kwako inaweza kuwa ni 11. Hivyo mnatakiwa kuishi kulingana na kile mlichotengeneza kwenye namba 1 hapo juu. Pia hukatazwi kujifunza kutoka fomula za watu wengine.

3. Punguza au acha kuwa na mawasilino na mpenzi au wapenzi wako wa zamani. Hili pia ni jambo zuri sana. Mawasiliano ya mara kwa mara na mpenzi au wapenzi wako wa zamani huondoa au kupunguza msisimiko kwa wanandoa. Pia hali hii hupunguza uaminifu katika Ndoa na kufanya Ndoa nyingi kuwa legelege.

4. Jitengenezee marafiki wengi wa Jinsia yako. Hapa pia watu wengi hufanya kosa kwa kuwa na marafiki wengi wa Jinsia tofauti. Kuwa kwako karibu sana na marafiki wa Jinsia tofauti hutengeneza hali ya wasiwasi kwa mwenza wako na kusababisha sintofahamu ambayo hufanya Ndoa kutokuwa imara.

5. Chunga sana Maneno na ushauri wa ndugu aumarafiki. Marafiki wengi hupenda kuharibu Ndoa za watu. Kuwa makini sana na Maneno unayo-ambiwa na ndugu au marafiki. Chekecha vizuri Maneno yao ili ufanye uamuzi ulio sahihi.

6. Chagua marafiki waliokuzidi umri na maendeleo pia. Hili pia ni jambo la msingi. Marafiki wa aina hii watakusaidia kupata elimu juu ya maisha kwa ujumla na kukufanya uzidi kisonga mbele kimaisha badala ya kurudi nyuma.

7. Kuvumiliana na kusameheana ni muhimu pia, kwasababu hufanya maisha ya Ndoa kuwa yenye furaha. Kumbuka Ndoa yenye Furaha mara nyingi huwa na maendeleo pia.


Kumbuka:
KUMCHA NA KUMTEGEMEA MUMGU KATIKA MAISHA YA NDOA NI MUHIMU SANA.

Karibuni kama kuna jambo la kuongezea pia tusambaze ujumbe huu.

Nawasilisha.
 
Raha ya ngoma ingia ucheze, na kila ngoma ina step zake.
 
Kama hujaoa au kuolewa huwezi kumshauri mwenye ndoa ABADAN

Jamii Forums mobile app
 
Hakuna mshauri wa ndoa hapo..ni Jesus tu wanadamu wote wanafiq tu
 
Hakuna mshauri wa ndoa hapo..ni Jesus tu wanadamu wote wanafiq tu
Inawezekana kwa mtazamo wako. Ila MUNGU ametuumba pia kwa lengo la kuwasaidia wengine kimawazo na mtazamo pia.
 
Back
Top Bottom