Mlendamboga
JF-Expert Member
- Sep 14, 2011
- 670
- 347
Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo utaratibu wa kurejesha mgao wa umeme kiaina, hali imeendelea kuwa mbaya siku hadi siku.Jana ofisi za serikali hasa zenye kutumia kompyuta zile zisizokuwa na standby generator imekuwa shida. Leo tena tangu saa 12 jioni gizani mwendo mdundo hii nini? Nazungumzia mkoa wa Mbeya, sijui mikoa mingine
na prof. muhungo alijinasib pia. aliahidi kwa mbwembwe huku akiwakejeli 'watu' ya kuwa hakutakuwa na mgao. hivi yupo wapi siku hizi? au 'keshatulizwa'? Lizaboni, MSALANI, ifweero, MwanaDiwani tujulisheni! dar kuanzia last week umeme unakatika hata kwa saa 12. hii nchi imekuwa kama jehanum, mateso sana. tanesco na washirika wenu #BringBackOurMoneyArusha, Mwanza, Shinyanga, Kahama, Mwanza na Geita hakuna umeme. Pia watu wa Dar nao wanalalamika. Mgao wa umeme umerudi wanaona aibu kutangaza maana Profesa Kikwete aliahidi mgao wa umeme kuwa historia
Nimepata taarifa kutoka kwa mfanyakazi wa Tanesco ilala na amedhibitisha huu ni mgao usio rasmi mpaka tupige kelele ndio utangazwe hii ndio tanzania
Huku wapi? Taja mkoa maana ninaorodhesha hapa, nimeshafikisha mikoa tisa (9).hata mm nimeshawashtukia huku nako giza tangu jana