Hii form ya Manchester City wangekuwa nayo Manchester United tungekoma!

20171214_102830.png
 
Manchester United ni brand kubwa sana ni zaidi ya timu ya mpira wa miguu uwanjani. ..japo mimi sio shabiki wa hii timu.
 
Mdogo mdogo watakuwa kama eseno na livapuli. Washasahau ile hali ya kunyanyua kwapa.

Sitakaa nimsahau kocha wa zamani wa livapuli ambaye kwa sasa yupo pale celtic. Aliswmaje unajua!?

United wajiandae kisaikolojia, maana njia wanayopita ndio wanayopita Milan ya Gang Chomba, aseno ya Wacha 1 na livapuli ya kina King Ngwaba na MosDef.
United imebaki brand tu.
 
Aliyeleta huu uzi kama si fans wa arsenal basi ni livapuli maana ndo mna hasira sana na man u kisa wanawafunga sana
 
Hivi mnakumbuka wakati ligi inaanza?

Man untd walianza kwa kila aina ya mbwembwe na kujipa majina kama wazee wa 4g na mengineo..

Enzi hizo striker wao Lukaku anafunga balaa, wakaanza kuwatukana kina Morata na wengineo waliowakosa kwenye usajili

Mwisho wa siku wakaanza kula kipondo, watu wanajipigia tuu, mara ghafla lukaku wao akageuka LIKUKU..

Najaribu kuwaza hapa hivi hawa Man untd wangecheza mechi 15 mfulululizo bila kufungwa hata mechi 1 kama Man city hata hii J.F si tungeiona ya moto, tungeweka wapi nyuso zetu kwa mbwembwe zao zile...?
Umeona mbali mkuu.
Hawa jamaa huwa wanacheza mpira kwa midomo badala ya miguu.
 
Back
Top Bottom