MADIBA MANDELA
JF-Expert Member
- Mar 2, 2014
- 503
- 398
Kwenye kampeni za uchaguzi 2015 UKAWA mlizunguka nchi nzima mkiaminisha watanzania kuwa kuna uwezekano mkubwa wa watoto wa kitanzania kusoma bure bila kuchangia chochote.Tena UKAWA mlifika mbali mkasema elimu itakuwa bure kuanzia vidudu hadi chuo kikuu.Mlifanya makosa sana maana mlifanya wenzenu wa upande wa pili wadakie hiyo sera kichwa kichwa bila kuifanyia hata research.Matokeo yake sasa hela hakuna elimu bure imekua mwiba kwa serikali isiyojua hasa kuwa kwa sasa tupo kwenye CAPITALISM ambayo kwa nanmna yoyote mfumo huu wa maisha unalazima kila kitu lazima kiwe COST SHARING.UKAWA narudia hii dhambi inawahusu na mkitaka iwatoke wadokezeni wenzenu mlikua mnamaanisha nini na kama mlikua serious waambieni wapi watoe hizo fedha tafadhali.(UKIONA BABA MKALI SANA NYUMBANI UJUE HAKUNA HELA) so kuna mambo mengine tunaumizwa simply ni kwa sababu kuna mizigo ipo na serilkali imeshindwa kabisa kuibeba.UKAWA UKAWA UKAWA mlitukosea sana tunaomba mtuombe radhi.