Hii dalili ya nini!

G M S

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
502
53
Wamember eti kupata makoozi yasiyoisha kwa mda wa zaidi ya miaka 2 ni dalili ya ugonjwa gani? Na je unatibika vp?
 
Mkuu TB inatibika kabisa tena ni bure kabisa gharama ni nauli tu ya kwenda kumeza dozi kilasi. Nenda kapime haraka kabla ijakomaa zaidi.
 
Wamember eti kupata makoozi yasiyoisha kwa mda wa zaidi ya miaka 2 ni dalili ya ugonjwa gani? Na je unatibika vp?


KUPATA MAKOHOZI KWA MUDA WA MIAKA MIWILI NI DALILI YA MAGONJWA NA SIYO UGONJWA LAKINI UNATAKIWA UANGALIE NA DALILI NYINGINE KATI YA HIZI NITAKAZO TAJA
Kukohoa kwa mda mrefu
kutoka jasho usiku
kupungua uzito
makohozi yana chembe chembe za damu au yana damu kabisa
Hizo hapo juu zaweza kuwa ni Kifua kikuu hasa kama unakuwa na homa ya kiwango cha chini na kutoka jasho usiku kapime ppd or makohozi.

PILI
kama unakohoa kwa mda mrefu
makohozi ni meupe kiasi
unakuwa na matatizo ya kupumua (difficult in breathing)
unakuwa na homa
mapigo ya moyo hayako kawaida
inawezekana ikawa ni COPD kwakweli sijui kuisema kwa kiswahili samahani kapige x-ray ya kifua pamoja na bloog gases

TATU
Kama una kohoa kwa mda mrefu
Makohozi yakiwa na damu
Unapungua uzito
na Hom hiyo yawezekana ni kansa ya mapafu kwa hiyo nenda kafanye x-ray then pima kansa marker utapata jibu kutokana na matokeo ya x-ray
au brochoscopy.

Nadhani hayo yatasaidia mkuu
 
Back
Top Bottom