PreGE2025 Hii battle kati ya VPN na mitandao ya kijamii ni balaa, tutafika Oktoba tukiwa tumechoka sana!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
2,786
Reaction score
7,567
Wakuu,

Hivi mnapitia kama nnachopitia mimi? Kwasababu natumia sana Telegram naazimika kutumia VPN ili mambo yaende baada ya kupigwa pini na wajomba.

Sasa kazi inaanza ukiwasha VPN unaweza kupata telegram lakini mitandao mingine inakata, ila usiku ukiingia mara nyingine (sio mara zote) Telegram inakubali bila VPN huku mitandao mingine unakuwa hutoboi bila VPN🀣🀣.

Ni kama vile kuna mtu ako na switch anaichezesha tu anavyotaka, naona hii ya mwaka huu itakuwa kali kuliko ya 2020. Inabidi uwe na VPN kama 3 hivi za akiba. Moja ikizingua unaswitch kwa nyingine, ikizingua unaenda kwa nyingine nayo ikizingua unarudi kwa ya mwanzo mzunguo unaanza upya

Ila mama 🀣🀣 mitano tena, mama ametufikisha, hana baya🀣🀣 mwaka huu tutaona kila rangi.

NB: Hakikisha hukosi VPN kama tatu kwenye simu, usije kulialia kazi zako haziendi, mara madili yamekwama, misukule ya mama iko bize kuhakikisha wote tunagalala kama Jenista Mhagama
 
Watu wana majeshi, polisi, TISS lakini bado wanaogopa watu kuchat Telegram
Unachezea maandanamo ya mtandao kwenye huoni sura za watu🀣🀣🀣
 
hata hivyo naona tayari ni wazi mmeshakata pumzi ya kijamii, kisiasa na kiuchumi mapeeema tena kwenye hatua za mwanzo tu πŸ’
 
hata hivyo naona tayari ni wazi mmeshakata pumzi ya kijamii, kisiasa na kiuchumi mapeeema tena kwenye hatua za mwanzo tu πŸ’
Nani sasa amekata pumzi Gentleman?πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Wanasiasa ni wajinga tu kuna mdau hapo anasema tatizo sio la Tz anasahau hata huko nje kuna wanasiasi pia na wapumbavu sanaa maana wanapenda kucontrol hizi social platforms ila mwamba ya Telegram aliwakataa sana.
 
Si ndio hapo, wanataka kushindana na teknolojia... ngoja tuone watafikia wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…