Hii bajeti ya kodi za Pombe toka nasoma hadi leo, hivi Gesi, madini yanafaida gani kwa Mtanzania?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,459
2,000
Haya ni baadhi ya maeneo yanayoonesha jinsi serikali itakavyokusanya kodi.

1. Vinywaji baridi imeongezeka kwa Sh3 kutoka Sh58 mpaka Sh61.

2. Maji ya kunywa imeongezeka kwa Sh3 kutoka Sh58 hadi Sh61 kwa Lita.

3. Juisi ya matunda ya ndani imeshuka kwa senti 50 kutoka Sh9.50 hadi Sh9 kwa lita.

4. Juisi ya matunda ya nje imeoanda kwa Sh11 kutoka Sh210 mpaka Sh221 kwa Lita.

5. Bia inayotengenezwa kwa nafaka ya ndani imepanda kwa Sh21 kwa Lita kutoka Sh429 mpaka Sh450.

6. Bia nyingine zote imepanda kwa Sh36 kutoka Sh729 mpaka Sh765 kwa lita.

7. Bia zisizo za kilevi imepanda kwa Sh27 kutoka Sh534 mpaka Sh561.

8. Mvinyo wa zabibu ya ndani imeshuka kwa Sh2 kwa lita kutoka Sh202 mpaka Sh200.

9. Mvinyo wa zabibu ya nje imepanda kwa Sh113 kwa lita kutoka Sh2,236 mpaka Sh2,349.

10. Vinywaji vikali kutoka nje imepanda kwa Sh166 kutoka Sh3,315 mpaka Sh3,481. Vinywaji vikali vya nchini itaendelea kubaki Sh3,315.

Katika eneo hili la vinywaji,serikali imeendelea kulitumia kama chanzo kikuu cha mapato ,wachumi wanasema eneo hili linachunguliwa kama anasa kama ilivyo kwa sigara!.

11. Sigara za ndani zisizo za kichungi imeongezeka kwa Sh593 kwa kila sigara 1,000 kutoka Sh11,854 mpaka Sh12,447.

12. Road license imefutwa
Wakati road license ikifutwa, ada ya usajili wa magari imepanda.

a) Injini ya 501-1500 cc kutoka Sh150, mpaka Sh200,000.

b) Injini ya 1501-2500 cc kutoka Sh200,000 mpaka Sh250,000.

c) Injini ya zaidi ya 2501 cc kutoka Sh250,000 mpaka Sh300,000.

13.Kupanda kwa bei ya mafuta kama petrol na disel kunakwenda ongeza gharama ya maisha,wakulima wote walioamia kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji wanakwenda bebeshwa mzigo wa kodi,

Leo vijana wengi wamewekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji,gharama zankuendesha mashine zinakwenda kupanda!

Watanzania wamefutiwa Road Licence,halafu wanapandishiwa gharama za usajili,pia gharama za kila siku za kuendesha maghari zimepaa!.

Hili lina hatari kubwa kuliko hata kufutwa kwa road licence,wabunge wasipokuwa makini,gharama za kumiliki maghari zinakwenda kuwa juu,nauli za
mabasi zinakwenda kupaa!.

Serikali imesema sasa madini hayatakwenda nje moja kwa moja bila ukaguzi,hapa wabunge wanatakiwa kuibana serikali sana,kwa nini haitaki kubadili sheria za kodi na uwekezaji zilizopitishwa kwa hati ya dharura mwaka 1997?.

Eneo hili ndipo tunapoibiwa sana,kwa nini serikali haitaki kuipitia upya sera ya madini ili kuimarisha fidia kwa wanaoamishwa kuwapisha wawekezaji,sheria hii ndiyo inayowakabidhi wawekezaji haki zote za kumiliki maeneo yenye utajiri wa madini!

Kauli ya waziri kuwa sasa madini lazima yakaguliwe bado haijatibu wizi kwenye sekta ya madini,ila angalau imeonesha dhamira kwa hatua za awali!

Kama umemsikiliza waziri vizuri,utagundua,jicho la serikali ni kwenye uchumi mkubwa na si uchumi mdogo!.
Tuendelee kuichambua bajeti yetu!
 

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
12,977
2,000
Hizi hela anazokamua Lukuvi kwenye manyumba ya watu mbona sizioni kwenye budget?

Na hela za minada ya ngombe na zile faini za wanaobeba mkaa kwa baiskeli wapi?

Ile 4% ya makinikia yenyewe inakuwa wapi? Hii budget ya kienyeji sana
 

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,589
2,000
Walevi wa pombe na wavuta sigara nao wamezidi sana..kila mwaka wanapandishiwa bei ila hawakomi wao wapo tu,natamani sigara moja iuzwe jero,na pombe bei rahisi iwe buku tano huenda wataacha,maana tumewachoka sasa
 

Napoleone

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
6,124
2,000
Nchi haina vyanzo vya mapato vya kiume kiume namaanisha vyanzo vyenye mashiko na ndomana imebakia kutafta fedha kwa mwananchi wa kawaida kwa kumkamua had ndururu yake,..taasis za serikal zenye dhamana kwenye madin,utalii,anga,maji,hazifanyi kaz yake,so hakuna jipya,no export,nchi inapataje pesa,.kutwa ku discourage sekta binafsi,mara toen pesa weken nmb,mara panden ndege za serikal tuu etc,nchi haiwez pata pesa za maana kwa kumkamua maskin wa chin kabsa na mfanyakaz,.vipaumbele vyetu havina mashiko,ma flyover,mara madege meng meng,.hiv haya mabilion yangewekezwa kwenye kilimo,yaan kuwe na projects za mabilion yaan ma plantation ya kufa mtu,mashamba makubwa ya mazao ya biashara kila mkoa,watu waajiriwe huko wakae vijana huko maelf na maelf na wajengewe viwanda huko vya kuboresha mazao tuanze ku export hizo bidhaa nje tupate foreign currency,lakin wap,kutwa budget za kusadikika,mwaka jana trilion 28 sjui 29 huko,zilizokusanywa ni tril 18 tuu kumi zote hakuna,.af tutegemee mabadiliko?
 

Baba Joseph17

JF-Expert Member
Jul 15, 2013
8,367
2,000
Hizi hela anazokamua Lukuvi kwenye manyumba ya watu mbona sizioni kwenye budget?

Na hela za minada ya ngombe na zile faini za wanaobeba mkaa kwa baiskeli wapi?

Ile 4% ya makinikia yenyewe inakuwa wapi? Hii budget ya kienyeji sana
Mbona haujauliza kodi kutokana na mauzo ya gesi hizo ulizotaja wewe zinakusanywa na wizara husika zipo kwenye kundi LA kodi za kisekta
 

Baba Joseph17

JF-Expert Member
Jul 15, 2013
8,367
2,000
Walevi wa pombe na wavuta sigara nao wamezidi sana..kila mwaka wanapandishiwa bei ila hawakomi wao wapo tu,natamani sigara moja iuzwe jero,na pombe bei rahisi iwe buku tano huenda wataacha,maana tumewachoka sasa
Wakiacha kodi itatoka wapi? We badala ya kusema tunywe sana ili kodi iwe kubwa unataka tukose kodi?
 

Ninaweza

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
9,821
2,000
Walevi wa pombe na wavuta sigara nao wamezidi sana..kila mwaka wanapandishiwa bei ila hawakomi wao wapo tu,natamani sigara moja iuzwe jero,na pombe bei rahisi iwe buku tano huenda wataacha,maana tumewachoka sasa
Na serikali ifirisike
 

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
47,137
2,000
Akiweka kodi kwenye madini, biss wako Lisu anakuja na povu kwamba atafukuza wawekezaji na anaweza kushtakiwa kwenye mahakama za kimataifa!
Wezi wa madini na gesi ni nyie wehu CCM ndiyo maana hamtaki mikataba iwe wazi.
 

Sophist

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
4,073
2,000
Serikali imesema sasa madini hayatakwenda nje moja kwa moja bila ukaguzi,hapa wabunge wanatakiwa kuibana serikali sana,kwa nini haitaki kubadili sheria za kodi na uwekezaji zilizopitishwa kwa hati ya dharura mwaka 1997?.
Hiyo ni sheria ipi ya madini, 1929, 1979, 1998, au 2010? Ninakushauri uwe unafanya rejea kabla ya kusajili malalamiko yako kwenye public.
 

Sophist

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
4,073
2,000
Wezi wa madini na gesi ni nyie wehu CCM ndiyo maana hamtaki mikataba iwe wazi.
all mining contracts (MDAs) are subject to public disclosure; acha uongo. Ninakushauri uwe unasoma nyaraka za sera husika kabla ya kutoa matamshi yako kwenye public.
 

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
3,288
2,000
Ninakuunga mkono kwenye suala la kutegemea pombe katika bajeti ya kuendesha serikali kila mwaka. Hata raisi wetu Dr John Pombe Magufuli alishasema hivi karibuni kuwa wachumi wetu wa mipango waachane na kutegemea hiyo kitu ya jina lake katika bajeti ya nchi yetu. Kwamba wanatakiwa wawe wabunifu zaidi. Sasa ni dhahili wamekaidi agizo lake kwa kuongeza tena bei ya hiyo kitu ambacho ni cha mhimu sana baada ya kazi!!! Yaani hawaogopi hata kutumbuliwa kwa kupandisha bei ya Pombe kinyume na agizo la mheshimiwa rais.
 

jabulani

JF-Expert Member
Aug 1, 2015
3,949
2,000
Kabla ya bajeti kwisha waruhusu watu kunywa bia muda wowote wanaotaka, hapo ndo wataongeza mapato ya kueleweka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom