Mungu mkubwa.Labda ana fununu fulani kutoka ICC, kuwa lile Simba Jike lishakua implicated! Ujue Warioba ana connection kubwa kule maana alikuwa Rais wa Mahakama ya Sheria za Bahari Duniani.
Polepole alimwamini sana Butiku akawa anampa info zote, ndio maana nimesema ngoja nibaki ndugu mtazamaji.pesa tamu labda anatafuta wengine akawauze
Mkuu uko mule mule, maana imekuwa ghafla mno kwa huyu mzee kubadilika ndio maana jana kagusia Chadema kufungiwa na Lissu kuendelea kushikiliwa.Mpango mzima (kwa jicho la pembeni)ni kwamba hiyo tarehe 22/01/2026, hao wazee watakaa na kutoka na kauli kwamba Lisu aachiwe, chadema ifunguliwe, Mchakato wa katiba na Tume Huru uanze na au uharakishwe ili kuondoa malalamiko ya wananchi.
Hawa wazee ni kama vile wanatuona hatujui ni mchezo gani wanataka au wapenga kuufamya.
Halafu serikali itatekeleza maazimio yao na kusema kwamba imewasikiliza wazee wenye Busara na ndicho ilicho kifanya- just to save face.
Haya mambo ya kesi ya Lissu na kufungukiwa kwa wapinzani- Lissu na Mpina, hayakutakiwa kabisa kutokea kabisa...
Nakubaliana na wewe kuwa Huyu Butiku sio mtu wa kumuamini kwani anatumia taasisi na jina la Nyerere kama kitega uchumi chake , na hana credibility tena kwa wa Tanganyika! Sio Siri kuwa kumsaliti Kwake Humphrey Polepole ni pigo kubwa sana kwa wazalendo wa nchi hii. Hata akatae vipi ukweli utabakia pale pale kuwa alimuuza kwa vipande vya fedha toka kwa Samia na hii ndio sababu ya kuweweseka kwake!Mimi ni Tomaso, hiki kigeu geu cha ghafla kinanitia wasiwasi, juzi alikuwa na wauaji leo anawatetea aliowasaliti juzi, je ni dhamiri yake au kuna msukumo wa nje au kuna project ambayo watawala wanataka waifanye kwa kutumia mgongo wake baada ya kushindwa kumshawishi Warioba.
Ni juzi tu alikuwa akiwananga vijana kuwa watoe hoja kwa utaratibu si maandamano, akawaambia hoja hazitatuliwi kwa kuharibu mali, ni juzi tu alisikika akimwambia Kapteni Tesha aliyewatetea vijana kuwa sio askari hana nidhamu ni muhuni.
Leo anawaambia vijana wana haki ya kuandamana, anawaambia watawala kuwa wasiseme hawawajui wauaji, anamwambia Katibu Mwenezi CCM kuwa anafanya siasa za hovyo, anawaambia CCM kuwa wanafanya siasa huku CHADEMA na mkiti wao LISSU wamewafungia kufanya siasa.
Wasiwasi ndio akili, ngoja niendelee kuwa tomaso hadi trh 22/1 atakapokutana na wazee wa Dar kina Kikwete labda nitaelewa lengo lake hasa ni nini.
Tunatakiwa kubonyeza button ya RESET TANZANIA ili tuanze upya.Nchi hii inatakiwa kuanza upya. Historia mbovu ya uasisi wa taifa hili iliyohusisha chama kilichoko madarakani, muungano unaofanana na ndoa za utotoni na taasisi zote za ulinzi wa raia na mipaka ya nchi vinatakiwa kuwekwa kwenye makumbusho ya taifa.
Tuweke misingi mipya ya utawala unaotii matakwa ya raia kama mwajiri wa watawala na vyombo vyake.