Hichi kinauzi hapa MMU

Jurrasic Park

JF-Expert Member
Sep 13, 2013
3,797
6,795
Habari

Hapa MMU kumekuwa na tabia ya baadhi ya memba ku-tag-ana wakati mtu anashida ya ushauri.

Wengine wanaenda mbali sana mpaka kuitana mashemeji, ba' mdogo, wifi, mjomba nk. unakuta uzi unajaa u ba mdogo na u shemeji ushauri hamna.

Wengine ni kusifiana jana walikuwa wanakula bata, wengine walipeana out, wengine walilewa, wengine waling'oa watoto wazuri na mengineyo. Mtu anataka ushauri lakini masihara mengi na utani usio na maana.

MAONI YANGU

Ingekuwa vizuri zaidi mkaanzisha uzi maalumu kama MAKAPUKU FORUM mkaachana na kuaribu nyuzi za wengine wanaohitaji ushauri.

Asanteni
 
Wenzako wanaitana shemeji, wengine ni mashemeji kweli. Raha ya MMU watu wanaweza kutafunana humu balaa.

Mleta uzi, humu kuna uwezekano wapo watu wanaenda zaidi ya 'urafiki', take it easy man!!!!

NIMEKUMBUKA UZI MMOJA

Memba mmoja kaomba msaada sasa badala ya msaada wakaanza kuitana ma ba mdogo, wifi, shemeji n.k ulienda mpaka page ya 30 hakuna ushauri wala nini ni ushemeji shemeji tu utafikiri wanajuana.

mbona kwenye nyuzi za magari hawaitani, intelligency ndo kabisa ila hapa sasa akiingia huyu jamaa Daby basi upepo unabadilika kabisa
 
Daaah MMU-Mahusiano....mapenzi au upendo na Urafiki Over asiyeelewa haambiwi maana
 
Humu kuna vitu ukisema uvichukulie serious utachukia bure vingine nikuvipotezea tu.
Ila mtoa mada unapoint sana tu japo wahusika watajidai hawazioni.
Hata kama ni kuitana hakuna anayepinga ila iwe kwa kiasi sio watu tunajisahau na kupoteza maana nzima ya uzi wa mtu.
Mtu anakuja na shida zake anategemea kupata ushauri ila sasa anajikuta alichotarajia kukipata sicho.
Nadhani kila kitu kikifanywa kwa kiasi hakileti madhara ila kitalapopitiliza kipimo hapo tatizo ndo linapoanzia.
Ila sometimes husaidia kuchangamsha uzi.
Kwa kiasi jamani msikere wengine.
 
Sasa mkuu unamind nini wakati jukwaa linajieleza , mapenzi, mahusiano na urafiki. Wewe unataka waitane vipi?
 
NIMEKUMBUKA UZI MMOJA

Memba mmoja kaomba msaada sasa badala ya msaada wakaanza kuitana ma ba mdogo, wifi, shemeji n.k ulienda mpaka page ya 30 hakuna ushauri wala nini ni ushemeji shemeji tu utafikiri wanajuana.

mbona kwenye nyuzi za magari hawaitani, intelligency ndo kabisa ila hapa sasa akiingia huyu jamaa Daby basi upepo unabadilika kabisa
Sasa kwenye huo Uzi wewe ulikuwa mtazamaji ???
 
NIMEKUMBUKA UZI MMOJA

Memba mmoja kaomba msaada sasa badala ya msaada wakaanza kuitana ma ba mdogo, wifi, shemeji n.k ulienda mpaka page ya 30 hakuna ushauri wala nini ni ushemeji shemeji tu utafikiri wanajuana.

mbona kwenye nyuzi za magari hawaitani, intelligency ndo kabisa ila hapa sasa akiingia huyu jamaa Daby basi upepo unabadilika kabisa
inaboa lkn ndo hvyo humu watu washakua ndugu tena daby ndo jf nzima ndugu zake.
 
NIMEKUMBUKA UZI MMOJA

Memba mmoja kaomba msaada sasa badala ya msaada wakaanza kuitana ma ba mdogo, wifi, shemeji n.k ulienda mpaka page ya 30 hakuna ushauri wala nini ni ushemeji shemeji tu utafikiri wanajuana.

mbona kwenye nyuzi za magari hawaitani, intelligency ndo kabisa ila hapa sasa akiingia huyu jamaa Daby basi upepo unabadilika kabisa
Mkuu nimegundua wazoefu na wakongwe wanapeana support
 
Uzoefu unaonesha kwamba katika jambo serious hicho unachokilalamikia hakitokei..

Ila ukileta Uzi wa mizaha na fiction ndani yake tarajia mizaha pia.

Issue sensitive ikipelekwa "chit chart" tarajia response ya hivyo hivyo.

Alafu humu ni stress free zone hebu acha RAIA tutiririke tupendavyo venye mtu anapenda mkulu kasema "tusipangiane"
 
Habari

Hapa MMU kumekuwa na tabia ya baadhi ya memba ku-tag-ana wakati mtu anashida ya ushauri.

Wengine wanaenda mbali sana mpaka kuitana mashemeji, ba' mdogo, wifi, mjomba nk. unakuta uzi unajaa u ba mdogo na u shemeji ushauri hamna.

wengine ni kusifiana jana walikuwa wanakula bata, wengine walipeana out, wengine walilewa, wengine waling'oa watto wazuri na mengineyo. mtu anataka ushauri lakini masihara mengi na utani usio na maana.

MAONI YANGU

Ingekuwa vizuri zaidi mkaanzisha uzi maalumu kama MAKAPUKU FORUM mkaachana na kuaribu nyuzi za wengine wanaohitaji ushauri.

Asanteni
Mjomba umeeleweka sema uvumilivu ni suala la msingi bamdogo... Ila vp shemeji hajambo?
 
Habari

Hapa MMU kumekuwa na tabia ya baadhi ya memba ku-tag-ana wakati mtu anashida ya ushauri.

Wengine wanaenda mbali sana mpaka kuitana mashemeji, ba' mdogo, wifi, mjomba nk. unakuta uzi unajaa u ba mdogo na u shemeji ushauri hamna.

wengine ni kusifiana jana walikuwa wanakula bata, wengine walipeana out, wengine walilewa, wengine waling'oa watto wazuri na mengineyo. mtu anataka ushauri lakini masihara mengi na utani usio na maana.

MAONI YANGU

Ingekuwa vizuri zaidi mkaanzisha uzi maalumu kama MAKAPUKU FORUM mkaachana na kuaribu nyuzi za wengine wanaohitaji ushauri.

Asanteni
mkuu nyuzi za namna hiyo huwa sicoment!

kuna watu wanajifanya Mmu ni ya baba zao kabisa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom