Ngosi
JF-Expert Member
- Oct 4, 2011
- 390
- 189
Hiari Scheme Ni Nini
Ni Skim mahsusi iliyoanzishwa na shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii kwa nia ya kutoa huduma za hifadhi ya jamii kwa watu walio katika sector isiyo rasmi, waliojiajiri wenyewe ,na wale walio katika mifuko mingine na wakapenda kujiunga kwa hiari.
Wanaohusika Na Mpango Huu
Mafao ya matibabu ya bure kwawanachama wa NSSF
Sifa
SWALI
Naomba mtu aliyejiunga na hii huduma anipe muongozo
Ni Skim mahsusi iliyoanzishwa na shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii kwa nia ya kutoa huduma za hifadhi ya jamii kwa watu walio katika sector isiyo rasmi, waliojiajiri wenyewe ,na wale walio katika mifuko mingine na wakapenda kujiunga kwa hiari.
Wanaohusika Na Mpango Huu
- Wanachama wote waliojiunga katika vikundi vya uzalishaji mali
- Mwanachama mmojammoja ilimradi awe na uhakika wa kuweza kuchangia japo Tshs. 20,000/- na kuendelea.
- Wanachama wote walio chini ya SACCOS na vyama vya ushirika nchini
- Wanachama wote wasio katika mfuko wa hifadhi ya jamii kisheria
- Wanachama walio katika mifuko mingine ila wakapenda kujiunga kwa mfumo wa hiari ili kupata mafao yatolewayo na NSSF.
- Wanachama wanaopata pensheni ya NSSF na wakawa radhi kukatwa asilimia sita(6%) ya pensheni yao ili kuweza kupata huduma ya matibabu
- Wakulima
- Wachimbaji wadogo wa madini
- Wavuvi
- Uandikishaji katika ofisi yoyote ya NSSF nchini.
- Uandikishaji katika maeneo ya biashara/shughuli zao kwa kuwaita maofisa wa NSSF
- Uandikishaji ni kwa njia ya Computer na kadi ya ki-electronikia yenye namba ya uanachama hutolewa.(SMART CARD)
- Mwanachama wa hiari/sekta isiyo rasmi atapaswa kulipa kiwango chochote ilimradi kisiwe chini ya Tshs. 20,000/- kwa mwezi na wale wachimabaji wadogo sh.50,000/-
- Michango hiyo itaanza tu mara mwanachama atakapoandikishwa.
- Michango hiyo hulipwa kila mwezi bila kuruka. Mwanachama akiruka mwezi/miezi itambidi alipie miezi hiyo ili huduma/mafao hasa ya matibabu yaendelee.
- Michango itapokelewa katika ofisi yoyote ya NSSF nchini na risiti itatolewa.
- Michango inaweza kuwasilishwa kwa mfumo wa simu M-PESA, TIGO PESA, NA AIRTEL MONEY kwa namba zitakazotolewa.
Mafao ya matibabu ya bure kwawanachama wa NSSF
Sifa
- Michango ya kuanzia miezi mitatu tu (3)
- Mume, Mke na Watoto 4 wenye umri usiozidi miaka 18 na 21 kwa wanaosoma
- Wastaafu watakaotaka huduma hii baada ya kustaafu.
- Kumuona daktari na huduma za uchunguzi
- Upaasuaji
- Huduma za dawa
- Huduma za rufaa kwenda hospitali za juu.
- Matibabu ya dharura nje ya vituo/hospitali aliyojiandikisha mwanachama.
- Wanachama wanaosafiri kikazi zaidi ya mara nne kwa mwaka nje ya mikoa yao
- Kulazwa zaidi ya siku 42 kwa mwaka
- Mwanachama Akifariki,
- Kuachishwa au kuacha kazi kwa mwanachama
- Kustaafu kwa umri
- Kutowasilisha kwa michango kwa miezi mitatu na
- Kufikia umri wa zaidi ya miaka 18 au 21 kwa watoto wa mwanachama
SWALI
Naomba mtu aliyejiunga na hii huduma anipe muongozo