Hezbollah wamekiri ameuawa

Hezbollah wamekiri ameuawa

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
18,355
Reaction score
26,852
Hezbollah wamekiri ameuawa

22 October, Israeli tena imerudia madai yake kwamba imemuua kiongozi namba mbili wa Hezbollah na mjumbe wa baraza kuu la Hezbollah bwana Heshem Safieddine mwanzoni mwa mwezi huu baada ya kimya kingi cha Hezbollah.

Hivyo Hezbollah jana ndio wamekiri kuuawa kwa kiongozi wao huyu mashuhuri aliyetarajiwa kushika nafasi ya hayati Hassan Nasrallah aliyekuwa kiongozi mkuu wa Hezbollah aliyeuawa mnamo 27 september.

Hashem ni binamu pia wa Hassan Nasrallah na kijana wake alimuoa binti mdomo wa jenerali wa Iran Qasem Suleman aliyeuawa na Trump mnamo 2020 na shambulio la drone huko Iraq.

Viongozi wakuu waliobakia katika Hezbollah ni Naim Qassem ambaye ndiye anayekaimu kiti cha Hassan Nasrallah pamoja na makamanda wengine wawili. Wote hawa wanatafutwa kuuawa.

Kuhusu vita

Vita bado vinaendelea, Israeli juzi imetangaza wakazi wa maeneo 25 wa jiji la Beirut waondoke haraka iwezekavyo ili wasiangamizwe kwa mashambulizi ya anga ambayo inayafanya sasa na yameleta uharibifu mkubwa wa mji huo na kuacha sehemu nyingi za mji bila wakazi.

Na zaidi kusini mwa Lebanon vita vya ardhini na anga vinaendelea na matokea yake ni wakazi wa Lebanon zaidi ya milioni wameyakimbia makazi yao.

Hezbollah pia wanajibu kwa kurusha makombora katika ardhi ya Israeli ukiwemo mji wa bandari Haifa. Jana wameushambulia pia mji wa Tel aviv kwa makombora manne, mawili yametunguliwa na mengine yamepenya.

Hezbollah imeonesha ukakamavu na imetoa changamoto kubwa mbele ya jeshi la Israeli hadi imefanikiwa kumuua kamanda wa Israeli anayesimamia kikosi maalum cha mapigano huko kusini mwa Lebanon.

Pia Israeli jana imefanya mashambulizi ya anga katika mji wa Dameski na Homs huko Siria na kuharibu maeneo ya kijeshi yanayotumika na Iran na Siria kama kambi za kuwafunza wanajeshi wa Hezbollah.

Vita bado ni mbichi ingawa uharibifu mkubwa upo upande wa Lenanon.

Na Jeff Massawe
 
Hezbollah wamekiri ameuawa

22 October, Israeli tena imerudia madai yake kwamba imemuua kiongozi namba mbili wa Hezbollah na mjumbe wa baraza kuu la Hezbollah bwana Heshem Safieddine mwanzoni mwa mwezi huu baada ya kimya kingi cha Hezbollah.

Hivyo Hezbollah jana ndio wamekiri kuuawa kwa kiongozi wao huyu mashuhuri aliyetarajiwa kushika nafasi ya hayati Hassan Nasrallah aliyekuwa kiongozi mkuu wa Hezbollah aliyeuawa mnamo 27 september. Hashem ni binamu pia wa Hassan Nasrallah na kijana wake alimuoa binti mdomo wa jenerali wa Iran Qasem Suleman aliyeuawa na Trump mnamo 2020 na shambulio la drone huko Iraq.

Viongozi wakuu waliobakia katika Hezbollah ni Naim Qassem ambaye ndiye anayekaimu kiti cha Hassan Nasrallah pamoja na makamanda wengine wawili. Wote hawa wanatafutwa kuuawa.

Kuhusu vita

Vita bado vinaendelea, Israeli juzi imetangaza wakazi wa maeneo 25 wa jiji la Beirut waondoke haraka iwezekavyo ili wasiangamizwe kwa mashambulizi ya anga ambayo inayafanya sasa na yameleta uharibifu mkubwa wa mji huo na kuacha sehemu nyingi za mji bila wakazi. Na zaidi kusini mwa Lebanon vita vya ardhini na anga vinaendelea na matokea yake ni wakazi wa Lebanon zaidi ya milioni wameyakimbia makazi yao. Hezbollah pia wanajibu kwa kurusha makombora katika ardhi ya Israeli ukiwemo mji wa bandari Haifa. Jana wameushambulia pia mji wa Tel aviv kwa makombora manne, mawili yametunguliwa na mengine yamepenya. Hezbollah imeonesha ukakamavu na imetoa changamoto kubwa mbele ya jeshi la Israeli hadi imefanikiwa kumuua kamanda wa Israeli anayesimamia kikosi maalum cha mapigano huko kusini mwa Lebanon.

Pia Israeli jana imefanya mashambulizi ya anga katika mji wa Dameski na Homs huko Siria na kuharibu maeneo ya kijeshi yanayotumika na Iran na Siria kama kambi za kuwafunza wanajeshi wa Hezbollah.

Vita bado ni mbichi ingawa uharibifu mkubwa upo upande wa Lenanon.

Na Jeff Massawe
Umeandika vzr..umegusa pande zote
Angalau ww nikobasi uliye na elimu
 
Back
Top Bottom