Hezbollah: Vita ya Gaza imeonyesha jinsi Israel walivyo dhaifu kuliko hata nyumba ya buibui

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,890
Hizbullah: Vita vya "Seif al-Quds" vimeonyesha kuwa, Israel ni dhaifu kuliko nyumba ya buibui

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imetangaza kuwa, vita vya "Seif al-Quds" vimeonyesha kuwa, utawala haramu wa Israel ni dhaifu kuliko hata nyumba ya buibui.

Taarifa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah iliyotolewa leo imetoa pongezi kwa ushindi wa makundi ya wanamapambano na wananchi wa Palestina baada ya utawala ghasibu wa Israel kukubali kusitisha vita bila masharti.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo ya Hizbullah ya Lebanon imesisitiza kuwa, wakati wa kujiri vita vya "Seif al-Quds' adui Mzayuni ametwishwa mahesabu mapya na kwamba, ushindi huu wa Palestina utakuwa na taathira kubwa katika vita na mapigano mengine katika eneo hili.

Kadhalika taarifa hiyo imebainisha kwamba, katika vita hivyo, wanamuqawama wa Palestina wamethibitisha kwamba, utawala ghasibu wa Israel una udhaifu na mapungufuu mengi katika nyuga mbalimbali za kijeshi na kiusalama.

Nembo ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon.

Wakati huo huo, wananchi wa maeneo mbalimbali ya ardhi za Palestina wamejitokeza mapema asubuhi ya leo kushangilia ushindi wa taifa hilo mbele ya adui Mzayuni baada ya kutangazwa usishaji vita.

Baada ya siku 11 za hujuma na mashambulio ya kijeshi ya utawala vamizi wa Kizayuni wa Israel hatimaye utawala huo umeafiki mpango wa kusitisha vita.

Baraza la mawaziri la utawala bandia wa Israel limekubaliana na mpango wa kusitisha vita na tayari usitishai vita huo ulianza kutekelezwa usiku wa manane kuamkia Ijumaa ya leo kwa majira ya Gaza.

Tags
 
Labda walitarajia wabaki watu wawili tu Palestine nzima
Haitokuja kutokea wakaisha, Israel hajui wapalestina kwa kuwapa ugumu wa maisha, wanabakiza starehe 1, nayo hupelekea ufyatuaji wa watoto kwa wingi. Wakati wao Waisraeli, wanaishi kibeberu, mtoto mmoja au wawili.

Cha Kanichekesha baada ya covid kuingia, wote walijifungia kimya, wanaogopa kufa kwa kirusi!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom