Yabesi Consult Co Ltd
Member
- Jan 13, 2018
- 38
- 60
Yohana 8:10
Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?
Ninaposoma habari hii ya Yesu na Mwanamke Huyu kuna maswali mengi ninayapata karibu kusoma Yh 8:2-11 kuna vitu utaviona.
Hawa ndugu walimkamata Mwana mama akizini wakamtembeza mitaa kwa mitaa wakimdharirisha kwamba Huyu mama ni kahaba wakiondoa Heshima yake kwamba yeye katika jamii hakustahili Heshima yote.
Licha ya kumtembeza barabarani lakini pia hawakueleza halikuwa Hanazini na Nani? hatujui yamkini Mwanamke Huyu alikuwa kahaba ndio maana hawakuangaika na yule baba aliyekuwa naye.
Ukitazama kwa makini utaona lengo lao lilikuwa ni kumwondolea Heshima Yule mama kwa kumtembeza barabarani pasipo kujali labda ana ndugu ana watoto wanaomtegemea NK
Hawa watu wakaona ili kuthibitisha matendo yao wakampeleka kwa Yesu tena wakijua kwamba kwa mujibu wa Sheria za Musa Mwana Mke kama Huyu anatakiwa kupigwa mawe afe ila hawakutaka kufanya hivyo walichotaka ni kumwona Bwana Yesu atafanya nini?
Unaposoma Yh 8: 8 tunaona Bwana Yesu anaandika katika Ardhi na alipokuwa aliandika tunaona kila Mmoja anahukumiwa nafsini mwake na kuondoka.
Yesu anatufundisha nini Yesu akikusamehe hata kama walikusema kwamba wewe ni muhaji Yesu akikusamehe wale waliokuwa wanakuita muuaji watakuheshimu watakuita majina yote mazuri. Mdo 9:2
Yesu akikusamehe hakuna jina baya ambalo utaitwa haijalishi wanakuita mchawi, haijalishi watakuita kahaba Yesu anabadilisha historia yako.
Unamfahamu Rahabu Yule kahaba wa Jos 2:2 Maisha ya Huyu Dada alipokutana na Yesu tunamkuta Yuko kwenye ukoo wa Yesu soma Mt 1:5
Ndugu yangu unangoja nini Leo hii ukisikia sauti ya Bwana usifanye moyo wako kuwa mgumu mpokee Yesu awe Bwana na Mwokozi wa Maisha yako akutengenze sifa njema.
Tafakari Maisha yako tafakari Tabia zako na sema na Mimi maneno Aya Ee Yesu naomba unisamehe Mimi Mwenye dhambi naomba unisamehe dhambi zangu zote naomba utengeneze Maisha yangu kwa upya naomba uandike historia yangu mpya kama ulivyofanya kwa Simon akawa Petro kama ulivyofanya kwa Sauli akawa Paul Fanya pia Kwangu katika Jina la Yesu Ameen.