Hesabu zinavyoipa ushindi CCM


Nimependa ushauri huu!! .
.
WANA CCM NISIKILIZENI..!!
Nina ushauri kwa wana CCM wenzangu; Lowasa kuhamia CHADEMA msipaniki. Kama kweli tulimaanisha kuwa hafai, ana uchu wa madaraka, alikiuka kanuni na maadili ya chama, ni mwizi na tena ni fisadi basi inabidi tushangilie kuondoka kwake, kwani kuvuja kwa pakacha sio ndio nafuu ya mchukuzi? Ila kama tulimkata kwa maslahi ya watu wachache na ikiwa tulitumia akili ndogo kulikata jina lake basi itabidi tujilaumu wenyewe kwa lolote tusilolitarajia litakalotokea.
Na tukiendelea kutumia akili ndogo za kudhani tutashinda kwa "magoli ya mikono", basi tunakwenda na maji mchana kweupe!
.
Tukijidanganya kuwa matusi, kejeli, mipasho, maneno ya kwenye kanga na nyimbo za Komba kwamba zitabadilisha huu upepo, pia tutajikuta tunakuwa chama cha upinzani bila hata kujiandaa kisaikolojia. Mwana CCM utakuwa unajichanganya kuushambulia uamuzi wa Lowasa kuhamia CHADEMA kwa sababu kimsingi CCM yetu ilishabariki vijana kadhaa wamshambulie majukwaani ili aonekane hafai na hao vijana wakazawadiwa vyeo. Mtu tuliemuona hafai kwetu inatuuma nini akiondoka kwetu? Ukioa mke kisha ukamtuhumu mbele za watu kuwa ni mzinzi na mshirikina; kisha mkaachana na akaolewa na mume mwingine, unaanzaje kuhangaika nae tena huko alikoenda? Tuwaache wapiga kura waamue kama ni sisi CCM ama UKAWA. .
.
Hata Mh. Mwenyekiti JK alishasema kila mtu ana haki kuongoza hii nchi; tunategemea kushinda lakini haitakuwa ajabu UKAWA wakitwaa madaraka kutokana na makosa yetu kimkakati. Wana CCM tusipaniki, kukomaa kisiasa ni pamoja na kuhimili na kukubali usichotarajia!
Wenu,
Mfurukutwa wa Shina.
😂😂👆
 
hizo ni opnion tu
je watu watapigia chama au mtu?
maana hao hao wajumbe wa nyumba 10 wa CCM wapo watakaompigia Lowasa! je data unazo? ama ni porojo?
uhakika ni kuwa october tutaona mabdaliko makubwa ya siasa za tanzania.
 
Kwenye hilo la vijijini, viongozi wenzangu wa UKAWA tusilibeze...yapo maeneo nchi hii bado upinzani hauna nguvu kabisa..naomba tujigawe tupeane majukumu kweli kweli ili kila kijiji na kitongoji nchii hii tutie Kambi tubadili fikra za watu hawa kuelekea ukombozi wa kweli. Hivyo tafiti hii sio ya kubeza hata kidogo
 
Mambo ya kudhani wanawake wanaisupport ccm yamepitwa na wakati. Wanawake kwa sasa nao mtindo mmoja UKAWA. Hata huko vijijini CCM imepoteza muelekeo,just wait 25 October

Nani aliyekwambia kuwa huko vijijin ccm imepotea fatilia matokeo ya serikali za mitaa ndo utajua kama ccm ipo au imepotea na ujue kama alivyosema asilimia kubwa ya wtz ni watu wanaoishi vijijini tofauti na asilimia chache ambao ndo wanaokaa mijini ccm kulingana na utafiti hapo juu uwezekano wa kushinda ni 100%ukubali au usikubali
 
Na wote tuliopo mijini ambapo tafiti inaonyesha UKAWA tunaikubali zaidi bila shaka asili yetu ni mikoani, hivyo tuwe tunawaelimisha ndugu zetu ambao wako vijijini huko...kila mtu akilifanya hilo ki uhakika zaidi tutaweza kuvuna kura nyingi kutokea huko....
 

Ccm mamluki ww baki huko huko na sera zko mbovu👈
 
Mambo ya kudhani wanawake wanaisupport ccm yamepitwa na wakati. Wanawake kwa sasa nao mtindo mmoja UKAWA. Hata huko vijijini CCM imepoteza muelekeo,just wait 25 October

nan kakudanganya?tena sasa hv wameamka kwa mwanamke kupendekezwa kua makamu wa rais,umoja wa wanawake ccm upo so powerfl compared na wa chadema unaongozwa na halima mdee,halima mdee hana convicng power kwa wanawake compare na viongoz wa ccm ambazo ni wamama watu wazima wanaokubalika..mf.sophia simba,asha roz migiro,i thnk ukawa u dnt hav 2 undrmine de power of dx group
 
Mambo ya kudhani wanawake wanaisupport ccm yamepitwa na wakati. Wanawake kwa sasa nao mtindo mmoja UKAWA. Hata huko vijijini CCM imepoteza muelekeo,just wait 25 October

Hao wanajichanganya hawafikirii kwa kina ona huyu bibi alichokiamua.na bibi kama huyu ndio waliokuwa wapiga kura wa kudumu kuichagua CCM

 
Last edited by a moderator:
familia yangu mbona haikuhusishwa kwenye uo utafit.. tupo 20 na tuna vikatio .. tumain letu ni ukawa.
 

Hadi migiro naye ana convincin power kubwa kuwezesha ushindi??
 

hivi unajua kwamba huko vijijini bado wanamkubali lowasa?
Na matumiz ya chopa yatasaidia kuzoa kura zote huko vijijini
 
hivi unajua kwamba huko vijijini bado wanamkubali lowasa?
Na matumiz ya chopa yatasaidia kuzoa kura zote huko vijijini

Hizo chopa ni za lowassa au ni za chama?? Gharama za kuhudumia hizo chopa zinatoka wap??
 
Hao wanajichanganya hawafikirii kwa kina ona huyu bibi alichokiamua.na bibi kama huyu ndio waliokuwa wapiga kura wa kudumu kuichagua CCM


Huyo bibi naye c ndo tunaosema walewale kwan ww umeona hyo na yule bibi anayemkataa lowasa kusema fisadi hujaiona mwaka huu mtalia na ukawa na lazma baada ya kushindwa mpotezane kisiasa cuf ishakufa ss baada ya uchaguz xx zamu ya cdm
 
Last edited by a moderator:
hivi unajua kwamba huko vijijini bado wanamkubali lowasa?
Na matumiz ya chopa yatasaidia kuzoa kura zote huko vijijini

Wtu wa vijijini hawafati mtu wanafata chama ww utawaambia nn wakati lowasa chama alichokwenda kijijin hakina umaarufu kivile tofauti na mjini
 
ingekuwa swala la utafiti ndo kigezo leo lowassa angekuwa mgombea wa ccm kwani tafiti zote zilionyesha anakubalika ndani na nje ya ccm cjawahi kuona tafiti inafanywa tu dar-es-salaam ndo ukawa utafiti wa Tanzania nzima bado tunafanya tafiti za officn si site
 
kama kawaida yenu ni waandishi wazuri wa makala, tukutane october

Huwo msemo wa tukutane Oktoba nimeanza kuusikia tangu mwaka 1995 kinachobadilika ni Mwaka tu lkn kila kitu kile kile!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…