Hesabu za gizani za Membe


muda ni lazima kwa huyu bwana maana anaona kila alichoanzisha hakifiki mwisho
 
Act agombee Membe, Chadema agombee Lissu au Nyalandu mwisho wa siku upinzani umepata kura nyingi ila wamezigawana so Ccm kama kawaida anaibuka mshindi. Ndo uzuri wa hesabu

Hilo ni iwapo rais aliyepo atakubali kuheshimu box la kura. Lakini kwa hali iliyopo, inaonyesha atatumia madaraka yake kupewa % anazozitaka.
 
NCCR Kama tawi la ccm kinaeza kupewa ushindi mezani ili kuleta mizania ya upande mmoja Bungeni... ie chama tawala ccm, chama kikuu cha upinzani ccm
ni mpango wa kuandaa mapapet wa kupiga muhuri siku ya kuongeza uda wa urais mpaka iwe miaka 20 subiri uone ngoma ni novemba tuu sio mbali sana
 
Nmekusoma vizuri sana!

Ila iwapo Membe ataenda ACT ccm watakuwa wamepiga hesabu zao vizuri, na huenda pengine ikawa ndio mpango uliopo wa ccm kumfanya Membe aende Act kwa lengo la kuibua chama kingine cha upinzani na kuipoteza chadema! Hii itakuwa inafaida kwa ccm.
 
Magufuli hana mpango wowote wa kuongeza muda, ila ni hofu yenu tu!

Kwa Membe kwenda ACT huo unaweza kuwa mpango kabisa wa ccm ukiwa na lengo wa kuinua chama kingine cha upinzani tofauti na chadema,.

Kama umemsikiliza vizuri Membe kwenye yale mahojiano na DW utaelewa!

Alafu kuna wajinga wachache hasa wapo huko upinzani wanakuona Membe ni mtu wa maana na wameshaanza kuweka matuamaini kwake. Sasa unajiuliza hivi Membe angekuwa mpinzani kweli wa Magufuli angeishia tu kubwbwaja kwenye twiter? Si angeenda kufuata form dodoma?
 
Tangu Magufuli aingie madarakani umeona mambo gani ya ccm aliyoamua yeye kama yeye badala ya chama kama chama?
 

CDM wanaamini kabisa, unaposema au kutaja jina la Membe, eti JPM hanywi kahawa wala maji!!!


CDM haipo, kuifanya iwepo lazima Membe atajwe tajwe sana


Sasa kumbe kuna NCCR na ACT, CDM unaiweka wapi?
 
Membe amepikwa akapikika katika uongozi.

Atatufaa sana akiwa rais.

Magufuli siyo rafiki wa wafanyakazi wala utawala wa sheria, apumzishwe tu!
 

Hawezi kuonyesha nia hiyo wazi wazi kwani kuna watu wengi hawaonyeshi kukubali hali hiyo. Ukiona kiongozi haheshimu box la kura, na anataka kuweka watu bungeni kwa utashi wake, hapo unapaswa kuusoma mchezo.

Ccm inaweza kuibua chama kingine cha upinzani zaidi ya cdm, kwani cdm ilipo ilinyanyuliwa kwa hisani ya ccm? Wananchi wameshaamka hivyo wanachagua watakacho, na sio ccm itakacho. Kwahiyo huko Zanzibar, CUF ilinyanyuliwa kwa hisani ya ccm? Acha kuleta consipirance theories.

Huyo Membe ana mvuto gani wa kukibeba chama chochote cha siasa? Wapinzani wanamshabikia kwakuwa anatengeneza tu mgogoro ccm, bila kujali ni wa kupanga au uhalisia. Huyo Membe tutampinga wazi wazi akija upinzani.
 
Tangu Magufuli aingie madarakani umeona mambo gani ya ccm aliyoamua yeye kama yeye badala ya chama kama chama?

Angalia tabia binafsi za Magufuli ndio zimebeba taswira ya ccm. Tabia ya kutoheshimu box la kura ni tabia binafsi ya Magufuli. Tazama toka ameingia madarakani chaguzi zetu zimekuwaje? Huo ni mfano mdogo tu, inahitaji akili ya wastani tu kutambua hili.
 
Mwache Membe kifo cha Mende asipotulia
 
Tanzania tunautamaduni wa kila awamu na chama chake kikuu cha Upinzani,

awamu ya Mwinyi tulikua na NCCR,awamu ya Mkapa tulikua na CUF na awamu ya Kikwete tulikua na CHADEMA , kwa awamu ya Magufuli basi atakua ACT.

hesabu ndogo tu hizi Mkuu
 
Unachosema; membe atasaidia tu kuongeza kura za majimbo ya kusini kuliko kushinda kiti cha urais. yawezekana lakini kusini kuna majimbo asiyoweza. Wapo akina Nape, Majaliwa, Hawa; Mhagama, n.k. ambao hatawamfuata, ng'o! Lete hesabu ya majimbo anayoweza kupata nafasi ni yapi?

Pia, elewa Membe hana umati kama ule wa Lowasa aliohama nao CCM. Membe yuko peke yake na kwa kiasi kikubwa anajulikana JF tu! Hajaondoka CCM na yeyote wa kumfuata. Waliohama na Lowasa walipata funzo baya kabisa! Waliyemfuata kawaacha huko yeye akarudi. Nani amfuate Membe?

Mwisho kwa mazungumzo ambayo amekuwa akiyafanya, siamini kama akili iko sawa. Membe leo hii anadai tume huru! Wakati aligombea urais kwa tume ile ile! halafu bado anaamini atagombea CCM! Akili haiko fresh!
 
Tanzania tunautamaduni wa kila awamu na chama chake kikuu cha Upinzani,

awamu ya Mwinyi tulikua na NCCR,awamu ya Mkapa tulikua na CUF na awamu ya Kikwete tulikua na CHADEMA , kwa awamu ya Magufuli basi atakua ACT.

hesabu ndogo tu hizi Mkuu
 
Membe sio mjinga kivile, anaweza akatengeneza zengwe ,au "akanogesha "uchaguzi mkuu wa October kwa kumpunguzia Magu wingi wa kura,kwa asili mia kubwa ili kumkata makali ya kujiamini.

Kwake majungu na fitina za kisayansi anayaweza kama jasusi mkongwe.Akiamua kujiongeza kwa kutumia mbinu za medani na fedha ya matajiri ni wazi atakidhalalisha chama cha Mapinduzi vibaya sana,japo Magu atatangazwa mshindi.
CCM wameshindwa kumpoza Membe mapema kabla ya uchaguzi.
 
Hivi unahisi ACT ikiwa na wabunge 10 chadema 2 hapo mpinzani mkuu ni yupi.?

Usichokijua wanachi mnatumika tu, kuzungushwa kuhama huku na kuhamia kule! Kwani unahisi pamoja na huko zanzibar kuwepo na upinzani, huo upinzani uko cuf kama awali?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…