Magufuli 05
JF-Expert Member
- May 7, 2023
- 1,990
- 3,821
Yanga ilikuwepo, ipo, na itakuwepo.
Usiku wa kuamkia leo umewakera wanayanga wengi kwa uamuzi wa kutoa mchango wa fedha kwa chama cha siasa. Yanga ina mashabiki kutoka vyama vyote vya siasa. Hata Chadema walipofanya harambee kama hii, klabu haikuchangia. Iweje leo klabu ichangie fedha nyingi kiasi hicho kwa chama cha siasa?
Sisi wanachama wa Yanga, ambao kwa sasa tunahamasishwa kuchangia tofali la ubingwa ili kuisaidia klabu kulipa madeni na kugharamia uendeshaji, tunaona ni matusi makubwa kuona sehemu ya michango yetu ikitolewa kwenda kwenye chama cha siasa hasa chama dola ambacho tayari kina kila kitu.
Tunatambua unafanya kazi nzuri, lakini Yanga haina chama; chama kina injinia, na injinia ana chama chake binafsi. Tafadhali tofautisha Yanga na injinia.
Hata kama tunataka kujenga kiwanja cha Kariakoo, hatupaswi kujipendekeza ili kupata eneo. Hata kama tulipata fedha za “Goli la Mama”, bado hatupaswi kujipendekeza.
FIFA inapinga vikali mambo kama haya. Kama wakituchunguza, tujiandae kwa lolote litakalotokea.
Brother, tafadhali sana, tenga klabu na CCM.