tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Rais wa Klabu ya Yanga, Hersi Said ameshindwa kupenya katika mchujo wa majina 13 ya wagombea ubunge Jimbo la Kongwa.
Hersi ameungana na wagombea wengine 11 ambao majina yao yameshindwa kupenya katika mchakato huo, huku aliyeshika nafasi ya pili kwenye kura za maoni Agosti 4, 2025, Isaya Mngurumi akipenya.
Soma pia: Ndugai huna chako Jimbo la Kongwa, Hersi Said wa Yanga ni Mbunge ajae Kongwa
Mapema leo, Katibu wa CCM Wilaya ya Kongwa, Joyce Mkaugala amesema jina la Hersi lilikuwa miongoni mwa makada 24 waliojitokeza kugombea ubunge wa jimbo hilo.
"Ni kweli Hersi ni miongozi mwa watiania wa nafasi ya ubunge ndani ya chama chetu, subirini taratibu zingine tutawajulisha, bado tunasubiri majina tuanze kampeni," alisema Mkaugala.
Hata hivyo, kwenye orodha iliyotolewa baadaye, jina la Hersi halikuwemo, sawa na la Mwalimu Deus Seif, mgombea aliyeshika nafasi ya tatu kwenye kura za maoni.
Hii ni mara ya pili kwa jina la Hersi kuondolewa kwenye mchakato wa ndani ya CCM katika majimbo mawili tofauti.
Awali, Hersi aliomba katika Jimbo la Kigamboni lakini majina ya walioteuliwa yalipotangazwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Amos Makala la kwake halikuwemo.