Heri ya siku ya kuzaliwa Diamond Platnumz

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,661
Tarehe 2/10/1989 Alizaliwa NASSEB ABDULLY JUMA a.k.a Diamond platumz simply unaweza muita Diamond! Kijana kafanya makubwa mengi ambayo hapa siwezi kuyasema kwasababu yanafahamika! kwa Lugha nyepesi naweza sema Jamaa Katutangaza watanzania kimziki nje ya Tanzania!

Pamoja na Mziki hata Kimapenzi Pia katutangaza nje ya Tanzania Baada za Kuzaa na mwadada maarufu na msaka pesa Zari The boss lady! Diamond Hakuna mafanikio yasiyo kuwa na changamoto, Changamoto unazipitia kwako wewe iwe ni somo na vishawishi vya wewe kujituma zaidi na zaidii kuhakikishia unafikia marengo yako! Hapa kwa leo nitasema mazuri yako tuu Japo binadamu hatujakamilika ila kwa Unachofanya kinatuburudisha sotee!

Naomba Mungu akusimamie kuendelea kufanya makubwa zaidii nikiingiaga shambani sa 12 asubuhi huwa naweka play list ya nyimbo zako hadi sa 12 jioni na hazichoshi hakika Unajua!

Kumbuka Diamond Uvumilivu,Kujituma nidhamu na kusali ni nguzo muhimu katika kufanikiwa! Katika Sala zako kumbuka kuwaombea hata wale wanao kunenea mabaya,Kukutukana na kukukashifu kwa juhudi zako Waombee Maisha marefu ili unavyobarikiwa wewe nao waoner baraka zako ulizopewa

Mtu akikupiga kofi la kushoto mgeuzie na la kulia! Maisha yako ni Mafundisho tosha kwa vijana wa sasa waohitaji kujifunzaa,kuto kukata tamaa ni Nguzo yako kubwaa! Be humble Diamond!

Binadamu ni Binadamu! mimi huwa nakuita wewe ni Mpambanaji

Hivyo sina budi kusema HERI YA SIKU YA KUZALIWA MPAMBANAJI DIAMOND

Wazungu wanasema HAPPY BIRTHDAY DIAMOND PLATNUMZ
 
I wish you could see what I see in him and the mission he is entrusted to accomplish. F. A. M. E is something else
 
Happy birthday MNYAMA ze real hustler....ubarikiwe sana mkuu na kuzidi kusonga mbele katika harakati zako
 
Back
Top Bottom