Heri ya Mwaka Mpya wa Serikali 2022/2023

Heri ya Mwaka Mpya wa Serikali 2022/2023

Mtu wa Asali

Senior Member
Joined
May 9, 2022
Posts
149
Reaction score
292
Dhima kuu ya bajeti itakayoanza kutekelezwa kuanzia siku ya leo ni “Kuongeza Kasi ya Kufufua Uchumi na Kuimarisha Sekta za Uzalishaji kwa ajili ya Kuboresha Maisha.”

Kufanikisha dhima hiyo, Mhe. Rais Samia Suluhu anaweka mkazo katika kilimo, mifugo, uvuvi, nishati, uwekezaji na biashara.
Kwa kufanya yafuatayo;

  • Serikali imeondoa kodi kwenye mafuta ya kula.
  • Serikali imepandisha mishahara kwa watumishi wa Umma

- Serikali imepandisha posho za kujikimu kwa Watumishi wa Umma.

- Imepunguza kodi kwenye ngano.

- Serikali imeanzisha mfumo mpya wa manunuzi unaozingatia bei halisi ya soko.

- Serikali Imetoa ruzuku ya bilioni 150 kwenye mbolea ya mazao ya aina zote

- Usahili wa kazi utakuwa kwa lugha ya Kiswahili

- Majengo yote makubwa na masoko makubwa yatakatiwa Bima.

- Punguzo la kodi la Zuio asilimia 5 kwenye Filamu.

- Ongezeko la mshahara Sekta binafsi

- Serikali imesamehe ushuru wa mazao kwenye mbegu.

- Mama amesamehe kodi kwenye Nyavu za kuvulia samaki.

- Wamachinga wametengewa bilioni 45 kujengewa miundombinu na kuwezeshwa.

- Serikali ya Mama imeondoa VAT kwenye mtindi (Yoghurt).
 
Ni mwanzo wa watu kula kwa urefu wa kamba zao na kulamba asali.
 
Rais amesha timiza wajibu wake.

Sasa kilicho baki ni watendaji na watekelezaji wa bajeti.

Endapo watendaji watashindwa au watasuasua kutekeleza Bajeti hiii basi hakuna budi kuondolewa mara moja ktk nafasi yake.

Uzoefu unaonyesha mara zote watendaji/watekelezaji ndio huwa wanakwamisha Bajeti mzuri kama hii. chondechonde tusiwafumbie watendaji wa ovyo.
 
Asante sana..ngoja tuzione ngonjera za walamba asali kwa mwaka huu nao.

Kikubwa ni ku low expectations..

#MaendeleoHayanaChama
 
Ccm ni wazuri kwenye karatasi ila kwenye kutekeleza ni wagumu na wavivu. Mfano hadi leo pikipiki ina bajaji ikishikwa faini inayotoka ni shillingi 30,000 wakati waliomba iwe 10.

Hapo kwenye mafuta ni kwa mafuta yanayozalishwa ndani. Mfano alizeti na pamba. Ila korie ambazo huagizwa nje in bulk before kusafishwa yataendelea kua na kodi
 
... hivi CCM kila mwaka wao ni KUFUFUA UCHUMI? Tangu baada ya Vita ya Kagera (Idd Amin), dhima imekuwa ndio hiyo! Huwa ni nani anaua uchumi halafu mwaka unaofuta shughuli inakuwa ni kuufufua?
 
... hivi CCM kila mwaka wao ni KUFUFUA UCHUMI? Tangu baada ya Vita ya Kagera (Idd Amin), dhima imekuwa ndio hiyo! Huwa ni nani anaua uchumi halafu mwaka unaofuta shughuli inakuwa ni kuufufua?
Tatizo lao wanabadirishana kila siku na kila mtu anakuja na wazo lake.
 
Ccm ni wazuri kwenye karatasi ila kwenye kutekeleza ni wagumu na wavivu. Mfano hadi leo pikipiki ina bajaji ikishikwa faini inayotoka ni shillingi 30,000 wakati waliomba iwe 10.

Hapo kwenye mafuta ni kwa mafuta yanayozalishwa ndani. Mfano alizeti na pamba. Ila korie ambazo huagizwa nje in bulk before kusafishwa yataendelea kua na kodi
Mada*aka ya kulevya.
 
Mwenye Enzi Mungu aendelee kuilinda nchi yetu Tanzania [emoji1241]
Atupe hekima, ufahamu, uwezo, afya , amani, upendo na utajiri wa hali ya juu sana sana walahi [emoji2972]
 
Back
Top Bottom