Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 5,759
- 7,573
Dunia hii ina watu wengi waliojaa machozi usoni, huzuni moyoni, na kukosa matumaini. Lakini kwa wale wanaomwamini Yesu Kristo, kuna ahadi yenye thamani kuu: "Heri ninyi mliao sasa, kwa sababu mtacheka." (Luka 6:21)
Yesu aliposema maneno hayo, pamoja na kuwafariji walioumizwa, alikuwa anawaonyesha picha kubwa zaidi ya maisha – kwamba siku inakuja mateso ya sasa yatakwisha na badala yake kutakuwa na furaha isiyo na mwisho katika ufalme wa Mungu.
Je, na wewe unalia sasa? Kama ndivyo, Mungu anaona machozi yako. Siku inakuja, machozi yako yatafutwa. Ahadi hiyo ipo katika Ufunuo 7:17.
Dalili zinaonesha wakati wa kucheka umekaribia. Yesu amekaribia sana kuja kulinyakua kanisa. Kuanzia siku hiyo wateule hawatalia tena bali watacheka na kufurahi milele na milele.
Yesu hakuishia kuwafariji waliao – aliinua pia sauti ya onyo kwa wale wanaocheka sasa katika dhambi. Katika Luka 6:25 anasema: "Ole wenu ninyi mnaocheka sasa, kwa kuwa mtaomboleza na kulia."
Hilo ni onyo la kutisha kwa wale wanaofurahia kufanya dhambi na kuona kana kwamba Mungu hayupo. Wanaocheka sasa kwa sababu wamezama katika uovu – kicheko chao kitageuka kuwa kilio kisicho na mwisho siku Yesu atakaporudi. Watabaki katika dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Mbaya zaidi, baada ya hapo, watatupwa katika moto wa milele pamoja na ibilisi.
Inawezekana unacheka sasa ukiwa kwenye baa, umelewa pombe. Huenda unachekelea kwakuwa umefaulu kuiba mke au mme wa mtu na kufanya naye uzinzi. Labda pia unacheka kwa sababu umefaulu kumtapeli jirani yako na kumuibia pesa. Au labda unacheka kwa sababu umesema uongo na kukwepa jambo fulani.
Ukicheka kwa sababu umefanya dhambi, hicho ni kicheko cha kujidanganya. Ni kama meli inayocheza juu ya mawimbi kabla ya kugonga mwamba. Ni hakika kwamba wanaocheka katika dhambi sasa, watalia kwa majuto yasiyokuwa na mwisho, Yesu akija.
Kama umetambua kuwa u miongoni mwa wale wanaocheka sasa kwa sababu ya dhambi, neema bado ipo. Yesu anakuita leo umwamini, ubadili njia zako, ulie sasa na kutubu, ili siku ya mwisho ucheke pamoja na watakatifu, vinginevyo utalia na kusaga meno (Lk 13:28).
Umeamua kuwa katika kundi gani? Wanaolia sasa au watakaolia na kuomboleza baadaye?